Site icon A24TV News

BREAKING NEWS !RISASI ZARINDIMA KWENYE GARI LA MBUNGE SENDEKA ANUSURIKA YEYE NA DEREVA WAKE

Mbunge wa jimbo la Simanjiro mkoani Manyara ,Christopher Ole Sendeka amenusurika kuuwawa baada ya watu wasiojulikana kuliahambuliangari lake kwa risasi mapema leo jioni hii.

Taarifa za uhakika kutoka Simanjiro zinaeleza kwamba Mbunge huyo pamoja na dereva wake wote wamenusurika baada ya gari lao kushambuliwa kwa risasi wakati wakiwa jimboni humo.

Baadhi ya mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wameeleza kwamba walisikia milio ya risasi ikishmbulia gari hilo kabla ya washambuliaji kutokomea kusikojulikana.

A24 inaendelea kufuatilia taarifa hizi kwa ukaribu zaidi na itakuletea taarifa za kina kuhusu tukio hili endelea kuwa karibu nasi.

Mwisho .