Site icon A24TV News

FAMILIA YA OMARI MSAMO YAILILIA JESHI LA POLISI KUHUSU KIFO CHA NDUGU YAO UTATA MTUPU

Na Mwandishi wa A24tv Arusha

Jeshi la polisi wilaya ya Karatu Mkoani Arusha limeingia kwenye msuguani mkali na familia ya marehemu Omari Msamo, aliyekuwa dereva wa magari ya watalii( derevaTours),aliyefariki katika mazingira ya utata,akidaiwa kuuawa kwa kipigo na askari hao baada ya kusimamishwa kwenye kizuizi.

Tukio hilo limetokea Machi 16 mwaka huu katika eneo la Manyara Kibaoni wilayani Karatu,baada ya marehemu kusimamishwa na askari waliokuwa kwenye kituo cha ukaguzi .

Kwa mujibu wa msemeji wa famili ya marehemu,Fredy Asey alisema kuwa walishtushwa na kifo cha ndugu yao kwani hakua na ugonjwa wa aina yoyote na kuamua kufuatilia katika hospitali ya wilaya Karatu alikokuwa amepelekwa kupatiwa matibabu.

Alisema taarifa ya uchunguzi wa daktari katika hospitali hiyo ilionesha kuwa marehemu alikufa kutokana na hali ulevi jambo ambalo liliwafanya ndugu hao kuomba mwili wa marehemu ufanyiwe uchunguzi upya kwa kushirikisha ndugu na daktari wanayemwamini.

“Baada ya ndugu yetu kupoteza maisha tulifuatilia uchunguzi wa kifo chake katika hospitali ya karatu alikokuwa amepelekwa,lakini tulishtuka baada ya kuarifiwa kuwa marehemu alikufa kwa ulevi wa pombe, ndipo tulipoamua kumleta katika hospitali ya mkoa Mt meru kwa ajili ya uchunguzi zaidi ,ambapo imebainika kuwa marehemu alikutwa na majeraha makubwa yanayoashiria kusababisha kifo chake”

Asey akiongea na wanahabari katika hospitali ya Mt Meru ,alisema kuwa mwili wa marehemu baada ya kufanyiwa uchunguzi ,daktari aliyechunguza aliwaeleza kuwepo majereha makubwa matatu ambayo pia yalishuhudiwa na ndugu wa marehemu,likiwemo jeraha linaoonesha kutobolewa na kitu chenye ncha kali kisogoni,kwenye paji la uso na ubavuni.

Msemaji huyo wa familia alisema marehemu baada ya kusimamishwa na askari hao waliokuwa kwenye kituo hicho cha ukaguzi kulitokea kutoelewa kati yao na marehemu hali iliyosabajisha askari hao kumshambulia.

Alisema baada ya tukio hilo askari walimchukua marehemu hadi katika hospital ya wilaya Karatu na baadaye ilibaimika kwamba marehemu amefariki dunia .

Asey ameiomba serikali kupitia vyombo vyake vya uchunguzi (sio polisi )kufuatilia kifo cha ndugu yao wanayeamini kifo chake kimetokana na kipigo cha polisi baada ya sintofahamu kutokea siku ya tukio katika kizuizi hicho.

“Majibu haya ya daktari wa Mount Meru hatuna shaka kwamba ndugu yetu aliuawa ila hatujaridhika na namna ambavyo serikali haijachukua hatua juu ya jambo hili.

Hata hivyo askari polisi aliyekuwa eneo la tukio (jina linahifadhiwa)alidai kuwa marehemu baada ya kusimamishwa aliteremka kwenye gari na kudongoka chini na wao walijaribu kuokoa uhai wake kwa kumkimbiza hospitalini lakini alifariki dunia akipatiwa matibabu kwa sababu alikuwa katika hali ya ulevi.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo na simu yake ya mkononi ilijuwa imiita bila kupokelewa na jitihada za kusaka ili kutoa ufafanuzi zinaendelea.

Ends..