Site icon A24TV News

Jamii Wilayani Siha yatakiwa kuendelea kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili

Na Mwandishi wa A24tv.

Serikali Wilayani Siha mkoani Kilimanjarowa imewakumbusha wazazi/walezi Wilayani humo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kikamilifu katika malezi ya Watoto na kuwalinda dhidi ya vitendo vya kikatili ikiwamo ubakaji na ulawiti pamoja na ndoa za utotoni vinavyoendelea katika jamii.

Hayo yamejiri wakati wa maazimisho siku ya wanawake Duniani ambapo kiwilaya yamefanyika katika ukumbi wa RC Sanya juu Wilayani humo na kuhudhuria na viongozi mbali mbali wa Serikali ,madiwani ,wadau wakupinga vitendo vya ukatili , Tasisi mbali mbali za Kibank ikiwamo Uchumi Bank

Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Christopher Timbuka akizungumza katika maazimisho hayo ,amesema ni wajibu wa wazazi au walezi kuhakikisha Watoto wanasoma vyema, wanapatiwa chakula,huduma za afya na kutokomeza mila kandamizi zinazopelekea kuwepo kwa ndoa za utotoni,ubakaji, ulawit

“Ni kweli jamii inatakiwa kuendelea kumlinda mtoto ikiwa ni pamoja na kujengea uwezo wa kupambana dhidi ya vitendo hivyo ili kuwa na Taifa nzuri lenye maadili’amesema Timbuka

Amesema kila siku utasikia kwenye vyombo vya habari kwamba huyu amebakwa huyo amelawitia Mara huyu amea mtoto hata kwenye Wilaya yetu haya yapo, sasa tukikaa kimiya tukiyafumbia macho tutakuja kuwa na Taifa la ajabu ,naomba tupambane kizazi kibaki salama.

Timbuka amesema kuanzia 2020 hadi 2024 yapo matukio ya Ukatili wa kingono yaliyoripotiwa 122 Wilaya hiyo na matukio 138 ya kudhuru mwili

Amesema kwa kuliona hili Serikali inaendelea kujikita katika kuhakikisha vitendo vya ukatili dhidi ya Wanawake na watoto vinatoweka kwa kutoa elimu kwa jamii.

Pia kuunda mabaraza ya ulinzi na usalama kwa mtoto,kama nilivyosema haya yote hayawezi kufanikiwa bila kuwa na ushirikiano kutoka kwa Wananchi na hasa nyinyi wanawake,tuwalinde watoto wetu tukimuomba Mungu awaepushe na Hawa watu waovu wasio na utu

Aidha amesema siku ya march 20 wanategemea kuwa na ugeni wa makamu wa Raisi Philipo Mpango ambapo atafika Wilayani humo na kuweka jiwe la msingi shule ya Sekondari ya wasichana kilimanjaro mchepuo wa sayansi,hivyo kuomba Wananchi kujitokeza kwa wingi

Pia amewataka Wananchi kujiandaa na mbio za Mwenge April 4 mwaka huu ,tujiandae kushiriki kikamilifu, Mwenge wa uhuru mwaka huu unakaulimbio inayosema swala la utunzaji wa mazingira na pia kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT , Wilayani humo Bertha Mlay,amewataka wanawake kujitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali katika uchanguzi uliopo mbele wa Serikali za mitaa, vijiji,vitongoji kwani kufanya hivyo ni haki yao ya msingi

Mwisho