Site icon A24TV News

Kampuni ya Balton yatoa mafunzi kwa wakulima zaidi ya 300.

Mwandishi wetu,Arusha.

Wakulima zaidi ya 300 kutoka mikoa ya Geita Iringa Mbeya Morogoro Mwanza Shinyanga na Tabora wamepatiwa elimu ya namna ya kuchagua mbegu bora zinazokinzana na athari za mabadiliko ya Tabianchi.

Mafunzo hayo yametolewa na wataalamu wa sayansi ya mimea Toka kampuni ya Balton Tanzania inayoingiza na kusambaza mbegu Nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Balton Tanzania Chris Keeping amewaambia wakulima hao kuwa kufahamu aina ya mbegu inayofaa kulima katika ukanda waliopo pamoja n kujifunza namna ya kudhibiti wadudu kuwasaidia kupata mazao mengi Kwa wakulima hao.

Amesema kuwa kufanya kilimo chenye tija hususani kipindi hiki cha athari ya mabadiliko ya tabia ya nchi kutapelekea kuwa na chakula cha kutosha nchini na ziada kuuzwa nchinza nje.

Mafunzo hayo ya siku tatu yanatolewa na kampuni ya kuuza mbegu ya Balton Tanzania KATIKA shamba darasa lililopo makao makuu ya kampuni hiyo Iliyopo Ngaramtoni ya chini jijini Arusha, kwa lengo la kuwasaidia wakulima kujua mbinu za kulima na kufanya uchaguzi wa mbegu bora zinazokinzana na magonjwa pamoja na athari za mabadiliko ya Tabianchi.

Mtaalamu wa sayansi ya Mimea Toka BaltonTanzania Chonya Wema amewaambia wakulima hao hawana budi kufahamu teknolojia mbalimbali za Kilimo Biashara ili wanufaike na Kilimo kuliko kutumia Kilimo cha mazoea ambavhonhakina faida..

Amesema wakulima hao wamefundishwa namna ya kuhifadhi Maji Kwa kutumia nailon ambayo hutiririaha Maji kidogo kidogo Kwa mmea, pia jinsi ya kuandaa kitalu nyumba na mbegu maalumu za kupandia eneo husika

Nao wakulima walio shiriki mafunzo hayo wameeleza manufaa ya elimu waliyo ipata pamoja na changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo

 

Khalifani Saidi…Mkulima Toka Mkoa wa Morogoro amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia sana kupanda mbegu zinazotoa mazao mengi na kumnufaisha mkulima.

“Mafunzo haya yatanisaidia sana Mie na wakulima wenzangu pale Mlali Morogoro kwani tumeona shamba moja la nyanya likiandaliwa vizuri na kupanda mbegu hizi basi linaweza kutoa mazao mengi na kuleta faida kubwa” alisema Khalfan

Merry Kisusange ni Mkulima Toka Mkoa wa Iringa anasema kuwa mafunzo hayo yamewajia KATIKA wakati muafaka kwani waliokuwa wanavuna mazao kidogo Kwa sababu ya kutofahamu mbegu Bora inayoweza kumnufaisha mkulima.

Mwisho