Site icon A24TV News

MAMA MARIAM MWINYI AGAWA TAULO ZA KIKE PEMBA

Na Mosses Mashala .

Mke wa Rais wa Zanzibar , Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation Mhe.Mama Mariam Mwinyi amezindua programu ya kugawa taulo za kike (Tumaini Kits) katika viwanja vya Jadida Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba 29 Machi 2024.

Aidha Programu hiyo inafadhiliwa na Shirika la UNICEF kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu Zanzibar, pamoja na Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) kwa usambazaji wa Taulo za kike 1000 Unguja na Pemba.

Viongozi mbalimbali wameshiriki akiwemo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa, Mkuu wa UNICEF Zanzibar Laxmi Bhawani na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib.

Mwisho.