Na Mwandishi wa A24tv .
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala iliyoboreshwa itasaidia kuandaa wahitimu wenye sifa zinazohitajika katika soko la sasa la ajira ndani na nje ya nchi
Prof Mkenda amesema hayo Machi 07, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Viongozi wa Wizara na Wahariri wa Vyombo vya Habari wenye lengo la kuwajengea uelewa juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo 2023 pamoja na kupitishwa katkka Mitaala iliyoboreshwa ambayo imeanza kutekelezwa katika ngazi mbalimbali za elimu
Waziri huyo amesema kuwa katika Elimu ya Sekondari tayari utekelezaji umeanza Kwa Shule za Sekondari za Mkondo wa Elimu ya Amali ambapo tayari shule 96 ambaoo kati ya hizo 28 za serikali na Shule 68 za shule binafsi
Prof. Mkenda amesema uamuzi wa kufanya napitio ya sera Elimu na Kuboresha mitaala ni kutaka iendana na mahitaji ya Sasa ambayo itamuwezesha mhitimu kupata elimu ujuzi zaidi badala ya hapo awali mwamafunzi alikuwa akisona nadharia zaidi
Waziri Mkenda ameongeza kuwa ili kufikia malengo ya kutoa Elimu ujuzi Kwa wahitimu Kwa kutumia mitaala iliyoboreshwa eneo la Walimu limepewa uzito Mkubwa ambapo pia katika vyuo vya Ualimu nako mitaala imefanyiwa maboresho ili kuwezesha kupata Walimu wenye sifa stahiki zinasaidia kumudu kufundisha wanafunzi wanaohitajika katika soko la ajira la sasa
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amesema serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele katika sekta ya elimu hasa katika Ujenzi wa miundombinu yhna kutoa mafunzo Kwa Walimu kazini.
Amesema hayo Machi 7, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo ameongeza kuwa kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mbali ya uwekezaji huo imefanya mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 na kuja na Toleo la 2023.
“Ndani ya miaka miwili tuliweza kufanya majadiliano na jamii ya Kitanzania kuweza kupata maoni na mahitaji ya Watanzania namna gani wanataka elimu yao iwe” amesema Nombo.
Kiongozi huyo amesema pamoja na kwamba zimetumia mbinu mbalimbali za kuelimisha umma wa Watanzania lakini bado wizara iliona umuhimu kukutana na kujadiliana na wahariri ili wapate uelewa wa mabadiliko yaliyofanyika ili waweze saidia katika kuwafikia Watanzania wengi zaidi.
Akiongea Kwa niaba ya Wahariri wa vyombo vya habari Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deodatus Balile amesema Elimu ya Tanzania ni lazima ijielekeze zaidi katika kuwezesha Wanafunzi kupata ujuzi
Mwisho .