Site icon A24TV News

RAIS DK.MWINYI APOKEA POLE KUTOKA KWA WAJUMBE WA KAMATI KUU WA ZANZIBAR

Na Mosses Mashala .

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa upande wa Zanzibar wakiongozwa na Mohamed Aboud Mohamed , Leyla Burhan Ngozi  na Muhandisi Nasri Ally kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Mwenyekiti wa CCM Taifa Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja .

Mwisho .