Site icon A24TV News

TANAPA,TCAA NA MASHIRIKA 14 WAANZA KUCHUKUA HATUA KUIMARISHA USALAMA WA ANGA NDANI YA HIFADHI

Na Lilian Kasenene,Morogoro

Shirika la Uhifadhi Tanzania(TANAPA) kwa kushirkiana na Mamlaka ya usafiri wa anga nchini(TCAA) na mashirika 14 ya ndege wameanza kuchukua hatua za kuimarisha zaidi usalama na usafiri wa anga ndani ya hifadhi za taifa baada ya idadi ya watalii kuongezeka kutumia usafiri huo ili kuzifikia hifadhi mbalimbali kwa shughuli za utalii.

Afisa uhifadhi mkuu anayesimamia viwanja vya ndege kutoka Tanapa Chritine Bgoya amesema hayo katika kiwanja cha ndege cha Kikoboga kilichopo kwenye hifadhi ya taifa ya Mikumi wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo washiriki 19 walihudhuria

Bgoya amesema wote kwa pamoja wamekutana kwao ili kutafuta majibu kulingana na usafiri wa sekta ya anga unavyokuwa na kuangalia jitihada mbalimbali za kukuza utalii, fulsa zimekuwa zikijitokeza lakini kumekuwa na changamoto ambazo kitaalamu wanapaswa kuzishughulikia ingawa matokeo hayawezi kuwa ya moja kwa moja,

“Tumekutana na wadau wanaofanya usafiri wa anga ndani ya hifadhi zetu,kulingana na jitihada mbalimbali za kukuza utalii na fursa zinapokuwa kuna changamoto zinakuwa zinajitokeza lakini kitaalamu zina majibu yake lakini majibu hayo hayapatikani moja kwa moja bila kuyajadili kama wadau,”amesema

Amesema huo ni utaratibu wa kawaida kwa kufuata miongozo ya kitaifa na kimataifa imekuwa ikielekeza kuwa katika hali kama hiyo ya ongezeko la ndege na abiria inawahitaji kufanya uratibu wa namna hiyo na kukutana kwao ni ili kuangalia kwamba kuna mambo yanayohitaji maboresho,suala la usalama linaweza likaongezwa kiwango, na ufanisi wa shughuli za anga.

Bgoya amesema katika kuhakikisha hili linaenda vyema chuo cha usafiri wa anga likawapatia mafunzo ya usalama wa anga kwa hifadhi 11 zenye viwanja vya ndege, na mashirika ya ndege yameeleza mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa mabadiliko na kwamba wote kwa pamoja wamekubaliana kuwa wanaenda kuwa na ukurasa mpya katika usalama wa anga katika hifadhi za taifa.

Mkaguzi kiongozi huduma za uongozaji ndege kutoka TCAA Rashid Khamis amesema mamlaka hiyo ina wajibu wa kuhakikisha watalii wanaotumia usafiri wa anga wanakuwa salama ili kuja kwa wingi na kuongeza pato la taifa ili kuunga mkono juhudu za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

“Tunajua utalii ni moja ya chanzo kikuu cha pato la taifa hivyo utalii lazima ufanyike katika mazingira rafiki na salama ili kuwapa imani watumiaji wa ndani na nje ya Tanzania,”amesema.

Naye afisa mwandamizi wa uhifadhi, hifadhi ya Mikumi Herman Mtei amesema kumekuwa na utalii mkubwa kwa sasa na hiyo ni kutokana na matumizi ya viwanja vya ndege kutumika na kwamba watalii wengi wanaona kutumia usafiri huo ni rahisi kwani wa nawafika kwa muda kwenye hifadhi nyingi.

Aidha alisema wao kama wasimamizi wa viwanja vya ndege kwenye hifadhi zao kupata mafunzo hayo kunasaidia kusimamia kwa ufanisi na utaalamu na hiyo inasaidia kupunguza hata ajali zisizokuwa za lazima.

Pia amesema wao bila kujua kwa umakini viashiria vya usalama na namana ya kudhibiti ingewawia ugumu katika kulinda, ama kufanya kazi yao..

Kutokana na uwepo wa ongezeko la viwanja vya ndege kwenye hifadhi za taifa za Tanapa mafunzo hayo yatasaidia wahidhafhi wanaosimamia viwanja hivyo kusimamia kwa uafanisi na kuongeza usalama katika viwanja hivyo na mitambo ya kuongozea ndege.

Kwa kutumia kanuni za viwanja vya ndege tanapa iliomba mafunzo hayo kwa wafanyakazi hao ili kuhakikisha wanafuata sheria, kanuni, na taratibu zilizowekwa na mamlaka ya usafiri wa anga Tanzania na zile za shirika kuu la usafiri wa anga dunia.

Mwisho.