Site icon A24TV News

Wadau wa elimu Siha watoa mawazo yao ili kuboresha elimu ndani ya Wilaya hiyo

Serikali Wilayani siha imewashukuru wadau mbali mbali wa elimu Wilayani humo kwa michango yao na kutoa hoja nzuri ya namna ya kuboresha elimu na kupambana na changamoto zilizopo ili elimu iweze kusongambele Wilayani humo

Moja ya hoja ni iliyopendekezwa ni kuazishwa kwa mfuko wa kuchangia elimu kwa ajili ya kuwapo posho walimu wa kujitolea ,baada ya taarifa kwamba kuna upungufu wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari Wilayani humo.

Haya yamesemwa katika kilele cha hitimisho juma la Elimu katika ukumbi wa RC Sanya mbapo changamoto mbali mbali ziliziibuka moja wapo ni upungufu wa walimu ,utoro baadhi ya wanafunzi , Wazazi kutochangia chakula shuleni, kutohudhuria mikutano shuleni na kutofuatilia nyenendo za watoto wao

Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka Akizungumza hitimisho juma hilo ambalo lilihudhuriwa na wadau mbalibali wa elimu wakiwamo Wazazi,wanafunzi,walimu,Madiwani , viongozi wa Dini,ametoa Shukrani kwa mapendekezo yao yenye lengo la kusongeza elimu mbele ambalo ni jambo bora

“Tumepata kwenye taarifa tasmini ya elimu,kwenye michezo kwa maana ya mashairi na maigizo na pia kwenye taarifa ya awali ya Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri pamoja na taarifa zote zilizofuata baada yake tunamshukuru kwa taarifa hizo ambazo zitafanyiwa kazi” amesema Timbuka.

Timbuka amesema moja ya mapendekezo la wadau hao ni mfuko wa elimu kutoka kwa Diwani wa kata ya miti mirefu Simon Shija ambapo amesema kuanzishwa kwa mfuko huo itasaidia kupata walimu watakaosaidia elimu kupanda kupata

Amesema amemshukuru kwa wazo hilokupitia kwa Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi wataangalia namna na utaratibu uliopo kutokana na miongozo ya Serikali iliyopo na baada ya hapo tutaleta mrejesho Kama muongozo unasemaje juu ya uchangiaji

Kwa upande wake Mkurungenzi Mtendaji wa halmshauri hiyo Haji Mnasi amesema wanamshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa namna alivyoitendea haki katika sekta ya elimu katika Wilaya hii,wamekupokea fedha mbali mbali kwa ajili ya miundombinu ya shule za Msingi na Sekondari

Lakini pia ameweza kuona changamoto mbali mbali ,ameona namna zoezi hili ufundishaji na ufundishaji wanafunzi na matokeo yake ,bado yanahitaji msukumo na ndiyo tukaona tukutane na wadau mbalibali , Wazazi, wanafunzi,walimu,Madiwani na Viongozi ili kuweza kufikia malengo ya kumwezesha mtoto kufikia malengo ya aliyokusudia ,Kuona ujumbe wa leo kwamba elimu ni haki ya mtoto mpe frsa

Tunashuru wadau mbali mbali wamewaza kuchangia na kutoa hoja nzuri hivyo tunatarajia kuwa na matokeo mazuri zaidi katika nyanja hizi za elimu katika shule zetu za Msingi na Sekondari

Amesema lengo la kilele cha hitimisho la juma hili la elimu ni utaratibu wa kila mwaka Kitaifa kuwa kila na wiki na majumuhisho ambapo wanaangalia changamoto mbalibali zimekuwa zikijitokeza hasa kwenye sekta ya elimu nakuzifanyia kazi

Diwani Simon Shija amesema changamoto hizo ikiwamo upungufu huo wa walimu zinarudisha jitihanda za watoto kupata elimu bora hivyo nilazima zitatuliwa , Serikali inatoa fedha nyingi kwenye miradi mbalibali wakati mwingine tuunge mkono

Awali afisa elimu Sekondari Naomi Swai katika taarifa yake amesema kunauhitaji wa walimu katika shule za Msingi na Sekondari

Amesema katika shule ya awali na msingi wanawalimu 397 na wanaohitajika walimu 666 na unaona upungufu 269,amesema kwa Sekondari mchipuo wa sayansi Kuna walimu 122 na wanaohitajika 221
Mwisho