Site icon A24TV News

Wakazi Wilayani siha mkoani Kilimanjaro,Wamshuru mbunge kwa kusaidia gharama za matibabu

Na Mwandishi wa A24tv Siha

Wananchi wa Siha mkoani Kilimanjaro Wamesema wana kila sababu ya kumpongeza mbunge wa Jimbo hilo Goodwin Mollel kwa kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa wagonjwa wanaozuiliwa Hospitali kwa kushindwa kulipa gharama za matibabu wanazodaiwa.

Mbunge wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro akisalimiana na Wakazi wa Sanya juu Wilayani humo

Haya yamejiri akiwa viwanja vya Rex Sanya juu, wakati wa ziara yake kuongea na wananchi na pia kusikiliza kero zao zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi

Wakizungumzia wakiwa katika viwanja hivyo wamempa kongole mbunge huyo kwa mchango wake wa hali na mali ambao umesaidia baadhi ya familia kuwatoa ndugu zao Hospitali kwa kudaiwa gharama za matibabu ambazo wameshindwa kulipa.

Wakazi wa Sanya juu Wilayani siha mkoani Kilimanjaro wakimsikiliza mbunge

“Mollel unaendelea kutatua changamoto za Wananchi kwa ikikutumia gharama zako ,sisi wakazi wa Siha tuna kila sababu ya kukupongeza si tuu kukupongeza na kukuombea ili Mwenyezi Mungu ae ndelee kusimamia yale maono mema kwa watu wa Siha yaendeleo kutimia”Wamesema Wananchi hao

Wamesema kwa kipindi akiwa madarakani shule mbali mbali ,vituo vya Afya pamoja pamoja barabara zinajengwa na zinaendelea kujengwa.

Mbunge akiwa na mtoto aliyemsaidia gharama za matibabu taasisi ya moyo

Lilian Malya mmoja ya Wananchi hao amesema mtoto wake wa miaka (7)alimpeleka kupata matibabu ya moyo katika Taasisi ya moyo ya Jakaya (JKCI) Dar esalaam lakini nilitakiwa kutoa sh, 22 milioni kwa ajili ya gharama za mtoto kwa na mtoto nilimjulisha mbunge na aliweza kujisaidia nashukuru sana

Lilian amesema pamoja na kusaidia gharama za matibabu pia ameahidi kumsomesha ni jambo la kumshukuru sana na Mungu amfanyie wepesi katika majukumu yake,hizi fedha ni nyingi ni msaada mkubwa amenisaidia na aendelee kuwasaidia wengine wenye uitaji.

Kwa upande wake Diwani wa viti maalumu Egger Nzao,amesema kwamba mbunge ameweza kuwasaidia wagonjwa wengi kwa kusimamia gharama za matibabu na kuhakikisha wale watu wanatoka Hospitali,

kwa namna ya kipekee tunampongenza anafanya kazi kubwa na aendelee kuwasaidia watu wa Siha mbali na matibabu anadhamini watoto zaidi kupata masomo,

Mbunge huyo amewataka Wananchi kumuunga mkono katika majukumu yake ya kuwaletea maendeleao Wakazi wa Siha ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya maendeleao

Mwisho