Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa usalama na afya mahali pa kazi Adelhelm James Meru ametembelea maonyesho ya mabanda katika viwanja vya General taya Jijini Arusha kukagua mabanda pamoja na kujionea majukumu ya utekelezaji wa vifaa vinavyo tumika mahala pakazi .
Akiwa katika viwanja hivyo Mwenyekiti James amefuraishwa na kona uwekezaji mkubwa uliowekwa katika vifaa vya kazi mahala pa kazi kutoka kiwanda cha A- Z ambapo amejionea vifaa mbali mbali vinabyo saidia watumishi katika kutekeleza kazi zao kwa uraisi pia kujikinga na ajali mbali mbali wanapo kua katika majukumu yao ya kila siku viwandani .
Kilele cha Maadhimisho ya kimataifa ya usalama na afya mahala pa kazini kesho tarehe 28 mwezi April ambapo mgeni rasmi ni Naibu waziri Mkuu,na waziri wa nishati Doto biteko .