Site icon A24TV News

Dc,Siha atoa onyo kwa Watumishi wanachelewa kazini

Siha,

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka,ametoa angalizo kwa Watumishi wa umma wanaochelewa kufika kazini na kuwataka Wananchi kutoa taarifa wanapoona jambo hilo ili hatua za kinidhamu ziwezo kuchukuliwa dhidi yao

Haya yamejiri kwenye mafunzo ya usambazaji na uwasilishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi , Watendaji wa Wilaya ya Hai na Siha yaliyofanyika katika ukumbi wa Rc Sanya juu Wilayani siha,ambapo baadhi ya Viongozi wa Dini walihoji kuhusu Watumishi wanaochelewa kufika kazini.

Mkuu huyo Akizungumza katika mfunzo hayo ya siku moja na kuwajumuisha Wakuu wa Wilaya Hai na Siha, Madiwani , Watendaji , Wenyeviti wa Vijiji, Watumishi na Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na Viongozi wa Dini kutoka Wilaya zote mbili, Amewata watumishe kwenda kasi ya Rais Samia Suluhuu Hassani na kuchelewa vituo vya kazi ni kurudisha maendeleao nyuma

“Ni kweli kuzingatia muda kazi maswala ya kuwahi kazini ,vitu kana hivyo naomba visiletwa kama malalamiko kwenye mikutano au vikao Kama hivi mnapoona toeni taarifa kwa Viongozi viwezevkufanyiwa kazi”Amesema Timbuka

Timbuka Amesema ,Vitu kama hivi vikitokea kwenye ofisi zetu za vijiji, Kata na Wilaya kwamba changamoto ya kuna watu hawawai ofisini ,anachelewa ni busara kutoa taarifa mapema ili viweze kushughulikiwa visibakie hivyo itasaidia

Amesema kuchelewa kwao kazini kunakwamisha mambo mengi ya maendeleao kwa Serikali na hata kwa Wananchi,mtu anafika ofisini mapema ili apate huduma arudi kwenye majukumu yake lakini anakaa muda mrefu Jambo hili sio nzuri kabasa na halitakiwa kufumbiwa macho

Hata hivyo amawashauri Watumishi hao wanzingatie muda wa kazi ,Sheria na taratibu ,muda wa kazi unafahamika saa moja nusu mpaka saa tisa na nusu

Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani hapa Amiri Mkalipa,amesema wamepokea ushauri wa Viongozi wa Dini,lakini katika utumishi ,wnaomba Viongozi wa Dini moja ya vipengele vikubwa kwenye Dini ni uadilifu ,msiache kusemea ,

Sasa Viongozi wa Dini na Watumishi wa umma siku ya ijumaa ,jumamo na jumapili,tunapokuja msikiti na Kanisa msiache tukaenda mtuambie Bibilia inasemaje kuhusu utumishi uliotukuka kwa uadilifu kwenye suala la nidhamu ,swala la uhajibikaji ,

Masheik msituache ikiwa mnapata nafasi ,kuna maandiko yapo ya kumuaandaa huyu ajekuwa mtumishi bora mfanye hivyo ili kuwa na Watumishi bora wazuri wenye nidhamu ,wenye uadilifu maendeleao yatakuwepo

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Nurudin Babu,Amesema lengo la semina hiyo ni kuwajengea uwezo Viongozi hao kutafsiri katika kupanga na kuelekeza kufutilia na na kuthamini utekelezaji wa sera na mipango yetu ya muda mfupi wakati na muda mrefu

Na kwa kuwa swala la kupanga mipango linaanzia vijijini hadi ngazi ya Taifa ,sisi tunaowajibu kuratibu swala nzima la upangaji mipango na program za maendeleao.

Kwa hiyo semina hii inatuongezea ujuzi na kupata udheefu wa namna bora ya kutumia matokeo ya Sense katika kutekeleza wajibu wetu wa matumizi sahihi ya matokeo ya sense yataweze,matokeo ya sense ya sita mipango jumuhishi kwa maendeleao endelevu

Kiongozi wa chama cha SAU , Wilayani humo Mdoe Yambazi amepongeza mafunzo haya na kusema kuwa yamempa uelewa wa kuendelea kuhakikisaha Wananchi wa Siha wanaiga hatua za maendeleao na kutaka yafanyike hata vijijini

Mwisho