Site icon A24TV News

Ded Hai amesema hawatakaa ofisini hadi kukamilisha ukusanyaji mapato

Na Bahati Hai,

Mkurungenzi mtendaji wa Halmshauri ya Hai mkoani Kilimanjaro Dionis Myinga,amesema wanahitaji kufanya jitihada kubwa zaidi kuhakikisaha kwamba wanafikia asilimia 100 ya ukusanyaji mapato ndani ya mwezi mmoja uliobakia wa mwaka wa fedha

Pia amesema atahakikisha Miradi ambayo bado haijakamilika iweze kwishi kabla ya mwaka huu wa fedha haujaisha.

Akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la madiwani cha Halmshauri kilichofanyika katika ukumbi wa Halmshauri hiyo, amesema atahakikisha siku zilizosalia ukusanyaji mapato wanafikia asilimia 100

“Ni kweli sasa tunahitaji kufanya jitihada kubwa zaidi kuhakikisha kwamba tunafikia asilimia 100 au zaidi ,huu mwezi mmoja uliobakia ,maana yake tumetangaziana kutoka ofisini ili lengo litimie”amesema Myinga

Myinga amesema Mpaka sasa siku ya leo anavyongea kwamba mapato yote kwa ujumla wamefikia sh,3.8 bilion kati ya makisio ya sh,4.2 bilion ,ambapo sasa ni sawa na asilimia 89 .7 , sasa tujipongeze kwa hatua tuliyofikia.

Nadhani ni hatua nzuri Ila na tunaendea na zoezi hilo lengo kamili litimie, hakuna asiyejua umuhimu wa mapato haya,sasa hivi tunazungumzia kujenga matundu ya vyoo,kujenga madarasa,vituo vya Afya, Hospitali,barabara na shughuli nyingine nyingi

Amesema kwa sasa kama nilivyosema zimebaki wa hiyo ndugu zangu tunaendelea na operesheni ya kukusanya mapato sehemu mbalibali ya wilaya ili kufikia lengo lilikusudiwa la kuleta maendeleao

La pili ni kuhusu Miradi kwenye Maeneo yetu,Miradi ambayo bado haijakamilika,maana yake tukimbizane iweze kuisha kabla ya mwaka wa fedha haujaisha ambapo bado Kama mwezi mmoja na siku kadhaa

Huu mwezi mmoja ndiyo unatakiwa kwa kweli tuonekane sisi tunakamilisha miradi ifikapo June mwaka huu itakuwa muda mzuri zaidi ,tusisubiri hadi mwisho.

Kwa hiyo hili nalo ni swala la Msingi sana,lakini kuna swala la hoja za mkaguzi wa ndani lakini pia la mkuguzi wa nje na hili ni swala la utendaji makini unaotakiwa kwenye shughuli zetu tunazozifanya

Kwa hiyo nadhani pia pale ambapo hoja zilijitokeza zipo maana yake tunataka tujibu haraka sana na kikao tunaanza June mwaka huu,kwa hiyo ndugu zangu tumeshatangaza hilo ni lamsing

Mkuu wa Wilaya hiyo Amiri Mkalipa,amesema kila mzigo unapokwenda mwisho ndivyo unazidi kuwa mzito,tuwaombe sana nguvu tuliyokuwa nayo mwanzoni ndiyo nguvu ambayo tunatakiwa tuendelee sasa,mwaka wa fedha umebaki mwezi mmoja na siku 10

Timu yako mkurungenzi mtendaji,Madiwani na Wenyeviti wa mitaa tusaidieni kwa sababu lengo la kukusanya mapato ya halmshauri lengo ili kila mmoja amepewa,kwa hiyo tuongeze nguvu ifikapo tarehe ya mwisho tuwe tumefika asilimia 100

Mwisho