Site icon A24TV News

DK.MWINYI AKUTANA NA ASKOFU MKUU WA ANGLIKANA DUNIANI WELBY

Na Mosses Mashala .

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kianglikana na Taasisi nyingine za dini kwa kudumisha amani na utulivu .

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana Duniani , Askofu Mkuu Justin Welby na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 11 Mei 2024.

Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Askofu Justin Welby kwa ujio wake Zanzibar.

Naye Askofu Justin Welby amempa pole Rais Dk.Mwinyi kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi

Vilevile ujumbe huo umempongeza kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar

Rais Dk.Mwinyi atashiriki kesho Ibada ya Maridhiano kutokana na madhila waliyofanyiwa Waafrika wakati wa Biashara ya utumwa katika Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini itakayoongozwa na Askofu Mkuu, Mhashamu Justin Welby.

Mwisho