Site icon A24TV News

ECLAT FOUNDATION YAAHIDI KUJENGA SHULE YA MSINGI KITONGOJI CHA IMBOPONG-MFEREJI-MONDULI.

Na Mwandishi wa A24tv.

Mkurugenzi wa Shirika la ECLAT FOUNDATION Mr Peter Toima Ameahidi kuunga mkono Juhudi za Wananchi wa Kitongoji cha mbopong -Mfereji -Wilayani Monduli kwa kujenga shule ya Msingi .

Mr Toima Ametoa Ahadi hiyo ikiwa ni siku Chache tu Baada ya Baadhi wa wajumbe wa kijiji hicho kumfuata na Kumuomba awajengee shule kutokana na wanafunzi Kutembea umbali mrefu takriban kilomita 20 kufuata huduma ,

Ambapo tayari kuna darasa moja la Awali katika eneo hilo lililojengwa na Mdau wa Maendeleo DANIEL POROKWA  na Katibu wa Aliyekuwa  waziri Mkuu wa Tanzania Hayati EDWARD LOWASSA kwa kushirikiana na Nguvu kazi za wananchi.

MR Toima Amesema Jamii inapaswa kujua umuhimu wa Elimu na ndiyo Maana wao kama ECLAT FOUNDATION wamejikita hasa katika ujenzi wa shule Katika Baadhi ya Maeneo Mkoani Arusha ,Manyara nk Ambapo ujenzi huo wa shule ya Msingi katika kitongoji cha mbopong itafikisha  SHULE 8 Wilayani Monduli.

“Kila jambo lenye Manufaa lazima liwe na subira tumelipokea ombi lenu na tutarudi hapa Kusema kurudi sio leo wala kesho lakini tutarudi tutakuja kwa Awamu na mwezi wa saba tutakuwa hapa kwanza kutoa Elimu ya Uzazi, mwezi wa Tisa tutakuja hapa na Wafadhili walione Eneo ili mchakato wa Ujenzi wa Shule uanze, hili tutaliweza na lengo letu kama ECLAT FOUNDATION ni kuzunguka maeneo yote ya Monduli.

Kwa Upande wake Daniel Porokwa Ambaye ni katibu wa Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Hayati Edward Lowassa, Amewaomba na kuwasihi Mashirika Mengine kuiga Mfano bora wa Shirika la ECLAT Foundation chini ya Mr TOIMA, kuwa na Tabia ya kuwasaidia Watu wanaowazunguka hasa katika huduma Ambazo ni hafifu katika eneo husika.

” Mimi niseme tuna mashirika Mengi sana Arusha hasa Wilaya hizi za Kifugaji ukienda ngorongoro wapo, Monduli wapo, Longido wapo, Simanjiro wapo ninaomba tuige mfano wa ECLAT Foundation kusaidia Jamii inayotunguzuka ili tuwe na Manufaa Mazuri na jamii hiyo , tutumie Fedha za wafadhili vizuri ipasavyo.

Aidha kwa Upande wake EMBAPA PAAYA Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mfereji Amesema Wazo la Kujengwa kwa shule hiyo ilitokana na Wananchi, kutokana na watoto kutembea umbali mrefu Lakini aliyefanikisha ujenzi wa Darasa moja la awali ambalo tayari wanafunzi wanalitumia ni DANIEL POROKWA na kushukuru kwa ujio wa Mzee Toima.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kwa upande wa Wananchi akiwemo Ngaput Enjee, na Mwenyekiti wa kitongoji hicho na wa kijiji  Wamesema ujio wa shule hiyo itapunguza idadi ya watoto wanaoozeshwa pamoja, Wengine kuacha shule kutokana na Umbali pamoja na kutumia nafasi hiyo kuwashukuru wote walioguswa na Ujenzi wa Shule hiyo hasa DANIEL POROKWA Kwa kuanza kuwajengea Darasa moja na kumshaushi Mzee TOIMA kukubali kulichukua swala hilo na kuahidi kujenga shule ya msingi Mbopong Kata ya Mfereji Wilayani Monduli Ambapo Darasa hilo La Awali kwa sasa lina Wanafunzi 180 Wanaosomea katika Darasa hilo Ambalo kwa sasa halijakamilika.

Mwisho .