Site icon A24TV News

ELIMU YA POLISI JAMII NYUMBA KWA NYUMBA KATA YA NGARENARO SALAMA

Na Geofrey Stehen Arusha .

Mkaguzi wa kata ya NGARENARO jijini Arusha Mkaguzi Msaidizi wa polisi TADEY TARIMO leo Tarehe 24/05/2023 amepita nyumba kwa nyumba katika mitaa ya Kambi ya Fisi na Darajani na kutoa elimu ya ulinzi na Usalama

Mkaguzi huyo amezitaka Familia kutokukumbatia uhalifu na badala yake watoe TAARIFA za wahalifu walio katika makazi yao pamoja na uhalifu unaotendeka katika makazi yao.

A/INSP TARIMO ameitaka jamii ya mitaa hiyo kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pamoja na mamlaka ya kudhibiti na kuzuia madawa ya kulevya nchini DCEA kwa kupiga namba ya bure 119 ili kutoa TAARIFA za wanaojihusisha na biashara hiyo HARAMU

Mkaguzi huyo ameendea kuzihasa Familia za mitaa hiyo kuepukana na matumizi ya pombe haramu ya Moshi maarufu kama GONGO kwani ni kosa kisheria lakini vilevile kujiepusha na madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya pombe hiyo haramu.

A/INSP TARIMO amewahasa wananchi wa mitaa hiyo kujiepusha na matumizi ya pombe ya kienyeji aina ya DADII hususan nyakati za asubuhi na badala yake wajikite katika kazi kwa ustawi wa Familia zao

Mwisho Mkaguzi huyo amekemea vikali tabia ya vijana kujazana maeneo ya pembezoni mwa mto Ngarenaro badala yake watafute shughuli za kufanya badala ya kupoteza muda.

Mwisho .