Site icon A24TV News

KAYA MIA MBILI (200) YANUFAIKA NA UMEME WA JUA (SOLA) OLMOTI -LONGIDO

Na Juliana . Arusha

Mkurugenzi wa Shirika la Maasai Stoves Ndugu Kisioki Moitiko Amewataka Wamama jamii ya kifugaji katika kijiji cha Elerai kitongoji cha Olmoti Longido Kutunza na Kutumia Vyema Sola / Majiko ya kisasa Alizozikabidhi kwa lengo la kulinda afya zao Juu ya Moshi utokanao na Matumizi ya Kuni.

kisioki Amesema hayo katika zoezi la Ukabidhishwaji wa Umeme wa Jua (sola) Kwa Kaya 50 kati ya 150 waliopo kwenye Malengo Waliokwisha kabidhiwa sola hizo na jumla kupelekea Idadi kufikia kaya mia  200.

Sambamba na Kukabidhi sola hizo  Kisioki Amesema Sola hizo zimekuja mara baada ya wanawake hao kujengewa Majiko ya kisasa ya kutoa Moshi nje , Na kuwapongeza kwa kuendelea kusimamia vyema Bank ya kinamama yaani vikoba wanaoendesha wanawake hao Ambapo Ametolea mfano mmoja wa kikundi yenye mzunguko wa Wiki 41 Ambayo hadi sasa wamekusanya zaidi ya Millioni 6.

Wakizungumza Mara baada ya kukabidhiwa Sola hizo Wanawake hao Wamemshukuru Mkurugenzi Kisioki Moitiko kwa kujali Afya zao na kuahidi kutunza na Kusema itakuwa msaada na kuongeza Hari  kwa Watoto wao kujisomea Majumbani

 

 

Mwisho .