Na Geofrey Stephen Arusha
Kliniki ya Malalamiko iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paulo Makonda, imeanza kuzaa matunda kufuatia mjane Maryam Yahya Husein Mkazi wa jijini Dar es salaam aliyedai kudhulumiwa mali za Marehemu mumewe, kupatiwa ufumbuzi.
Maryamu alileta malalamiko yake mbele ya Mawakili kutoka chama cha Mawakili Tanganyika TLS, wanaosikiliza kero mbalimbali za wananchi katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa na kueleza namna anavyohangaishwa kupata haki ya mali za marehemu muwe licha ya kushinda kesi mahakamani mara kadhaa akipambania haki yake.
Akiongea katika viwanja hivyo mara baada ya kupatiwa msaada wa kisheria, Maryamu alisema aliolewa na marehemu aliyemtaja kwa jina la Ahmed Shariff kama mke wa pili na kujaliwa kupata naye watoto wawili.
“Nimekuja hapa nikitokea jijini Dar es salaam mara baada ya kusikia tangazo la Mkuu wa mkoa Makonda akisaidia wenye shida na wenye malalamiko mbalimbali nashukuru mungu nimesaidiwa kwa haraka sana ,mimi nimedhulumiwa mali za marehemu mume wangu na ndugu zake,kila nikishinda kesi wanakata tufaa”
Alisema mwaka 1918 mumewe alifariki dunia na kuacha mali kadhaa zikiwemo Nyumba za wapangaji zilizopo katikati ya jiji la Arusha .
Alisema baada ya kifo cha marehemu mumewe ndugu wa marehemu walitokea na kuzuia mali zote za marehemu wakisema mimi sikuwa mke wa marehemu ,nilikuwa mfanyakazi wa ndani jambo ambalo niliamua kwenda mahakamani.
“Nilifungua kesi mahakama ya mwanzo nikashinda wakataka rufaa mahakama ya wilaya nikashinda ,wakatata rufaa mahakama kuu nikashinda ,sasa chaajabu kila nikishinda wanakata rufaa na mpaka sasa wamekata rufaa nyingine mahakama ya rufaa na sijui kesi hii itaisha lini miaka sita sasa nahangaika na haki ya mali za marehemu mume wangu”
Maryamu alimshukuru mkuu wa mkoa wa Arusha kwa utaratibu wake aliouanzisha wa kusikiliza kero za wananchi,aliomba wakuu wengine wa mikoa kutumia utaratibu huo ili kuwasaidia wananchi wengine wanyonge kwa kuwa wenye shida ni wengi na hawana pa kukimbilia.
Tangu Makonda ameanzisha utaratibu huo wa kusikiliza kero na malalamiko ya wananchi ,Mei 7 Mwaka huu zoezi hilo la siku tatu limekuwa na mafanikio makubwa huku wananchi zaidi 2000 wamejitokeza wakiwa na madai mbalimbali
Mwisho.