Siha,
Mkuu wa jeshi la Polisi Wilaya siha mkoani Kilimanjaro Zakia Shuma,ametaja Askari wa jeshi hilo Wilayani humo kulinda mali za jeshi hilo zilizotolewa na Serikali ili ziweze kudumu bila kuchakaa mapema na kufanyakazi zilizokusudiwa za kulinda raia na mali zao
Sambamba na hilo Wadau mbali mbali wa maendeleao kuunga mkono na kutoa michango ili kuweza kukamilisha Ujenzi wa jengo jipya la Polisi kituo cha Sanya juu Wilayani humo kutokana na yale ya zamani kuwa chakavu.
Haya yamesemwa leo na Mkuu huyo wa jeshi la Polisi Wilaya humo baada ya kupokea gari aina ya Land Cruiser lililokuwa kwenye matengeneza ambapo lilikaa uko takribani mwezi mmoja na nusu, nakutoa rai za kulindwa mali hizo zinazotolewa na Serikali
“Napenda kutoa Rai kwa jeshi la Polisi hasa magereva hizi mali za Serikali mfano tumepewa gari,tujaribu kuyatunza kwa lengo la kudumu na kurahisisha ufanyaji wa kazi,tunapojua kuyatumia tujue pia na kuyatunza ili jambo zuri amesema Shuma
Zakia amesema Gari lilikuwa limeharibika sana marekebisho yalikuwa makubwa ,Sasa hivi limekuwa zima hivyo kuongeza nguvu za kufanya Doria nyakati za usiku na mchana maeneo ya Wilaya yetu.
“Ni kweli lilikuwa limeharibika sana linatumika na Mkuu wa upelelezi wa Wilaya ,limekaa uko takiribani mwezi mmoja na nusu,hivyo Tunawashukuru wadau mbalibali walioshiriki katika matengenezo akiwamo Ibrahim Motors wa Moshi mjinikwa moyo wao na tuendelee na ushirikiano huo ili kuleta maendeleao “amesema Zakia
Pia kupitia jeshi la hilo anatoa shurkurani za dhati kwa Wananchi kwa kushirikiana na jeshi hilo kufanikisha kupunguza uhalifu katika Wilaya hiyo,pia kwa Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleao ndani ya Wilaya hii
Kwa upande wake Furaha Mwakijila Mkuu wa polisi jamii Wilayani amewaomba Wananchi kuwaunga mkono kwa kutoa michango ili kukamilisha ujenzi wa jengo jipya la Polisi kituo cha Sanya juu,ili Askari pamoja wateja wanapofika kituoni kuhudumiwa wajisikie wapo salama.
Hivyo tunawasii Wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutuunga mkono kwa kutoa michango hiyo ili kukamilikasha ujenzi huo ambao upo hatua za mwisho,kwani ukiangalia majengo yanayotumika Sasa Ni ya zamani na yamechakaa kutokana na kituo hicho kujengea miaka mingi iliyopita
Daniel Nyolobi Baadhi ya Askari wamefurahishwa kwa ujio wa gari hilo na kusema litawarahishia kufika katika matukio kwa wakati Maeneo mbali mbalibali ya wilayani humo na pia kuahidi kulitunza gari hilo
Mwisho