Site icon A24TV News

RAIS MWINYI KUFUNGUA MKUTANO WANAHISA BANK YA CRDB JININI ARUSHA BANK YAPATA FAIDA BILIONI 428.8 WANAHISA KICHEKO

Na Geofrey Stephen ,Arusha.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kufungua semina ya wanahisa wa  benki ya CRDB  mei 17 mkoani Arusha.
Hayo yamesemwa leo mkoani Arusha na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Dkt. Ally Laay  wakati akizungumza  na waandishi wa habari mkoani Arusha.
Dkt.Laay amesema Mkutano Mkuu wa Wanahisa utatanguliwa na Semina ya Wanahisa itakayofanyika  Mei 17 huku ikifuatiwa na mkutano mkuu utakaofanyika mei  18.
Amesema kuwa ,maandalizi ya mkutano huo tayari yamekamilika huku akiwataka wanahisa kufika kwa wingi katika semina hiyo ambayo italenga  kujadili  ajenda mbalimbali .
Amesema kuwa,kupitia mkutano huo wataweza kujadili yatokanayo ambapo pia kitakuwa na gari la 2023 na kupanga mahali na sehemu ya kukutana kwa ajili ya mkutano ujao .
“Benki ya CRDB tumefanikiwa kupata faida ya shs bilioni  428.8 kwa mwaka 2023 kutoka shs bilioni 351.4 kwa mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 21 na hiyo ni baada ya kodi. “amesema Laay.
Amesema kuwa ,kutokana na mafanikio hayo makubwa walipendekeza gawio kuwa shs 50 kwa kila Hisa kutoka shs 45 iliyokuwepo hapo awali.,huku  kauli mbiu ikiwa ni “ustawi pamoja “.
Amefafanua kuwa, wanaendelea na mikakati mbalimbali ya kujitanua ndani na nje ya nchi ambapo wameshafungua matawi Burundi,DRC Congo ,ambapo wana mpango wa kwenda Zambia,Uganda,na nchi zingine za jumuiya  ya Afrika Mashariki na ukanda wa kusini.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela amewahamasisha kuhudhuria Semina na Mkutano Mkuu ikiwa ni haki yao ya kimsingi na kisheria lakini pia ushikiri wao unasaidia kuongeza tija na ufanisi katika uendeshaji wa Benki ya CRDB.
Nsekela amesema kuwamkutano huo ni muhimu sana kwa lengo la kuboresha huduma zinazotolewa  na benki hiyo na watatafakari mwaka wa kwanza wa utendaji wao na kuangalia namna walivyojipanga.
Ameongeza kuwa, benki hiyo wanasimamia vizuri utoaji wa mikopo kwa wanawake ,ambapo wameanza kurasimisha vikundi na kuviingiza  kwenye mfumo rasmi na kuanza kuwapa mikopo kidigitali.
“hii no benki ya kwanza  na ya kipekee nchini inayojali vijana wenye ubunifu kwa kuwasaidia katika maswala mbalimbali ili.waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza biashara zao.”amesema .
Ameongeza kuwa ,wamekuwa wakitenga asilimia moja ya faida yao kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii.
Katika mkutano huo pia Benki hiyo imetumia fursa hiyo kuzindua rasmi taarifa ya mwaka ya Benki pamoja na Ripoti ya ustawi endelevu (Sutainability Report) ambazo zinapatikana kwenye tovuti yetu.
Mwisho.