Site icon A24TV News

SERIKALI KUENDELEA KUAMINI WATANZANIA KATIKA KUEKEZA SEKTA YA MADINI ! MAPATO YAPAA JUU RAIS SAMIA AMELETA MABADILIKO MAKUBWA

Na Geofrey Stephen Arusha

Waziri wa Madini Anthony Mavunde amesema sekta ya madini hapa Nchini imefanikiwa kuongeza  ukuaji wa pato la taifa kutoka asilimia 5.1 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 9.1 mwaka 2023.

Waziri Mavunde ametoa kauli hiyo mapema leo wakati alipokuwa akifungua jukwaa la tatu la utekelezaji wa ushirikishwaji wa watanzania katika sekta ya Madini linalofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Aicc jijini Arusha.

Kutokana na mafanikio hayo serikali  imeongeza  bajeti katika sekta ya madini kutoka sh,bilioni 89 hadi sh,bilioni 231 na fedha hizo zimeelekezwa kwenye utafiti zaidi  wa madini na kuboresha maabara kwa lengo la kukuza sekta hiyo.

 

“Katika mwaka wa fedha 2024/25 unaoanza Januari mtashuhudia ujenzi wa maabara kubwa ya kisasa mjini Dodoma na mchakato wa ununuzi wa helkopta kwa ajili ya kufanya utafiti wa kina wa madini kwani hadi sasa utafiti umefanyika kwa asilimia 16 na lengo ni kufikia asilimia 50 ifikapo mwaka 2030”

 

Hata hivyo alisema sera ya madini ya mwaka 2009 ilisababisha malalamiko mengi kwa watanzania  juu ya ugumu wa kushirikimojak wa moja katika sekta ya madini.

Alisema wizara  ya madini inatekeleza mtazamo wa kufikia asilimia 50 ya utafiti wa eneo la madini nchi nzima ifikapo 2030.

Mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yametoa fursa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuhakikisha Watanzania wananufaika na rasilimali madini”Alisema Mavunde 

Katika hatua nyingine Waziri Mavunde alisema mwaka wa fedha uliopita 2022/23  serikali ilifanikiwa kukusanya maduhuli ya sh,bilioni 678 baada ya kufanyika  biashara ya madini yenye thamani ya sh, trilioni 1.7 katika vituo 100 vya manunuzi  na masoko 42 na kuchangia upatikanaji wa fedha za kigeni zaidi ya asilimia 56 

Mwisho .