Site icon A24TV News

TARURA Siha waomba fedha kiasi cha sh,733.9 milioni kukarabati miundombinu iliyoharibiwa na mvua

Na Mwandishi wa A24tv.

Siha,Baraza la Madiwani Halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro,limeomba Serikali kupitia (TARURA)isaidie kukarabati miundombinu mbali mbali ya barabara zilizoharibiwa vibaya na mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kusababisha gharama za usafiri kuongezaka

Pamoja na uharibifu wa miundombinu hiyo pia baadhi ya mashamba ya wakulima yamejaa maji na kuharibu mazao ikiwamo mahindi na maharage, hivyo kufanya baadhi ya Wananchi kukosa chakula cha kutosha.

Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancani Urasa akisoma taarifa katika kikao cha kawaida cha Baraza hilo lilifanyika katika ukumbi wa halmshauri,Amesema hali ni mbaya mvua hizo zimekata kabisa mawasiliana baadhi ya maeneo

Amesema kwa kipindi hiki cha mvua za masika zimeleta athari kubwa katika mashamba mazao kuharibika ,miondombinu ,baadhi ya majengo ya shule za Msingi na Sekondari na Maeneo mengine ya kijamii Kama vile ofisi za kata ,vijiji na Maeneo ya magulio

Pia zimeharibu barabara za vijijini na kusababisha usumbufu kwa Wananchi kushindwa kusafiri na kumsafirisha mazao ya kilimo na biashara ikiwa Ni pamoja na gharama za usafiri kupanda

“Ni kweli gharama za usafiri zimeongezeka labla mtu alikuwa atumia shilingi 5,000 analazika kutumia shilingi 1,5000 kutoka na barabara kuharibika na wenye vyomo vya Moto kupandisha gharama kutoka na kuzunguka umbali mrefu kutafuta sehemu nzuri ya kupita”Amesema Dancani.

Kutokana na hilo tunaomba Serikali itusaidie kukarabati miundombinu ya barabara zilizoharibiwa vibaya katika maeneo mbalibali Wilayani humo

Kuna barabara kutoka kwa Mkuu wa Wilaya kuelekea Karansi ,Tank la maji alafu kuelekea KIA na kutoka Sanya Juu kwenda KIA hizi zote zipo Tanroad Sasa zinaharibika hatuoni mtu akipita na kuzifanyia tathimini kwa hiyo tusaidiwe

Zipo barabara ambazo zipo chini ya (TARURA)ambazo madiwani wamazijataja zimeharibika vibaya zimegeuka mitaro ya kupitishia maji ,kwa kweli hali ni mbaya gharama za usafiri zimepanda,mvua ni neema lakini ndiyo hivyo.

Awali Juma Jani Diwani wa Kata ya Sanya juu,alitaka kufahamu baada ya mvua kunyesha na kuharibu miundombinu mbali mbali upi mpango mkakati wa kurudisha mawasiliano kwenye barabara zote

Kwa upande wake Meneja wa (TARURA), Wilayani humo Protas Kawishi,Amesema kwamba kuusiana na hali za barabara zilivyo sasa baada ya kunyesha mvua kubwa za vuli na masika barabara zimeathirika

Amesema kuna sehemu zinaharibika zaidi na mawasiliano yamekatika ndiyo sehemu tutatilia mkazo ili angalau huduma ziweze kupatikana japo kwa kusuasua ,Kama maeneo ya Karansi hasa barabara ya mawasiliano Magadini barabara ya Kadashi na Shengai ,daraja la Sekirari Mungushi na Maeneo mengine.

Kawishe Amesema wakati utaratibu wa kuboresha maeneo mengine unakamilika
wameandika barua kwenda Makao Makuu ya Tarura kuomba fedha kiasi cha sh,733.9 milion,kwa ajili ya jambo ,barabara zilizopo chini ya Tanrod mwandikieni Mkuu wa Wilaya kumjulisha

 

Mwisho