Site icon A24TV News

VIJANA WANAO LALA STOO YA SOKO KUONDOLEWA SANYA JUU KWA VITENDO VYA UBAKAJI NA ULAWITI .

 

Na Mwanfishi wa A24Tv .Siha,

Wananchi wa kata ya Sanya juu Wilayani siha mkoani Kilimanjaro,wameomba Serikali kufanya msako katika Soko la Sanya juu ili kuwaondoa vijana wanalala kwenye stoo za kuhifadhia mizigo na kufanya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji na ulawiti

Mbali na kufanya vitendo hivyo vya ukatili pia wamekuwa wakitumia dawa za kulevya ikiwamo bangi na mirungi hivyo kuathiri nguvu kazi ya Taifa

Wananchi hao wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti,wanesikitishwa kundi hilo na vijana kuishi sokoni hapo nakuomba Serikali kufanya masako huu hasa nyakati za usiku,ili kunusuru kizazi na kubaki salama.

“Ni kweli tunasema kunusuru kizazi kwa kupaza sauti kwa sababu vijana wanaofanya hivi vitendo ni kuanzia miaka 15 hadi 30 ambayo ndiyo nguvu kazi ya Taifa kukaa kimya kwa namna moja ni Kama kuunga mkono mambo hayo”Wamesema Wananchi hao

Jullias Mmar anasema vijana hao wamekuwa wakiishi kwa makundi kwenye stoo za kuhifadhia mizigo na nyumba moja iliyopo pembezoni mwa soko hilo wamekuwa wakifanya vitendo vya kikatili ikiwamo ubakaji na ulawiti na wakati mwingi wakifanyia vitendo hivyo wao kwa wao ,sio jambo la kufumbia macho

Akitolea mfano vijana hao hivi karibuni wamekuwa wakimlawiti Mara kwa mara kijana mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 35 ambaye ana matatizo ya akili mpaka wakina mama Wafanyabiashara wa soko hilo walipopaza sauti za kuondolewa vijana hao

Hawa vijana kipindi cha nyuma serikalini ilifanya msako na kuwaondoa ,Sasa wamerudi tena ,tunaomba wenye hizo stoo za kuhifadhia mizigo waulizwe kwanini wanaruhusu watu wengi kulala sehemu moja

Fadhila Ibrahim Mfanyabiashara wa Soko hilo ameitaka jamii kuungana kupiga vita vitendo hivyo vya kikatili na utumiaji wa dawa la kulevya hasa kwa vijana ili kujenga Taifa lenye heshima na kupata viongozi boro

Tukikaa kimya na tukafumbia macho mambo haya tutakuja kuwa na Taifa la ajabu sana ,watoto wadogo wanatumia dawa hizo la kulevya wanaingiluana kinyume na maumbile

Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha SanyaJuu Wilaya humo Wema Gasino ,amesema atalifanyia kazi jambo hilo,

“Talifanyia kazi hawa vijana awali tuliwatimua naona sasa wamerudi tena ,tutawaondoa hatuwezi kuvumilia uchafu huu”amesema Wema

Mwisho