Siha,
Halmshauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepewa kongole kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato ya ndani ambapo kwa sasa imefikia asilimia 93
Mbali na hilo pia ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), inaonyesha kwamba halmshauri siha imepata hati safi.
Muwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Gasper Ijiko Akizungumza kwenye kikao cha kawaida Baraza la hilo kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo,Amesema Siha ni miongoni mwa Wilaya inayo upa Mkoa nafasi nzuri kwenye ukusanyaji wa mapato.
“Nipongeze Halmashauri kwa ukusanyaji mzuri wa mapato,kama ambavyo mnafahamu tumepewa mkakati na maelekezo ya ukusanyaji wa mapato ya serikali na tunaangaliwa kwa kila robo na hivi sasa tunakwenda kuanza kuangaliwa kwa kipindi cha mwaka mzima”Amesema Ijiko
Ijiko Amesema ukusanyaji wa mapato kwa mkoa huu,Wilaya hii imekaa katika nafasi nzuri,mpaka sasa wapo asilimia 93 kwa robo tatu ya mwaka,tunaamini kama ilivyokuwa mwaka jana watafanyia kazi eneo hiyo na kuhakikisha ile historia iliyodumu kwa miaka Mitatu 3 ya ukusanyaji wa mapato vizuri itaendelea kudumu.
“Ni kweli tunaamini kama ilivyo mwaka jana ,hata mwaka huu halmshauri itafikia asilimia 100 kwa hiyo naamini Madiwani na kama mlivyokuwa mnasisitiza na Mkurungenzi Mtendajj muendelee kushikamana ili ile rekodi ya miaka mitatu mfululizo ya kufanya vizuri muendelee kubaki hongereni”alisisitiza Ijiko.
Amesema suala la pili ambalo nataka kuzungumza nikupongeza,tumepokea taarifa ya Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG),na katika ripoti hiyo imeonyesha kwamba halmshauri ya siha imepata hati safi ,hongereni hii pia ni rekodi nzuri kwa Baraza hili
Lakini pamoja na kupata hati safi ,kwa kawaida ile hati inaambatana na Maeneo yanayotaka kufanyiwa kazi ,kwa hiyo Kuna Maeneo tumehojiwa ,hoja za kufanyia ukaguzi,kwa hiyo naomba tufanyie kazi zile hoja za ukaguzi ambazo tumezipata ili ziweze kufungwa
Awali Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Dancani Urasa katika taarifa yake Amesema kwa kipindi cha robo ya tatu takwimu zinanyesha ukusanyaji mapato ya ndani yamefikia asilimia 93
Hata hivyo ametoa wito kwa Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri Haji Mnasi na Wataalamu wake kuendelea kuweka nguvu kwenye ukusanyaji wa mapata ili kufikia lengo lilikusudiwa.
Mack Masua kwa niaba ya Mkurungenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo Haji Mnasi,amesema wataendelea na ushikiano na kuaidi kutekeleza yale yote yaliyoshauriwa
Mwisho