Site icon A24TV News

Bodi ya maji Lawate Fuka Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro imepokea mita 20 za maji za kulipia kabla

Na Bahati Siha

Siha ,Serikali imetoa mita 20 za majaribio za kulipia kabla kwa Bodi ya maji Lawate Fuka Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro

Mita hizo zimetolewa kwa lengo la kuongeza kipato kwa Taasisi na pia kupunguza malalamiko kwa wateja ambao bao udai ya kubambikiwa bili za maji.

 

Meneja wa bodi hiyo Elihuruma Masawe Akizungumza na waandishi wa habari walipofika kwake,Amesema umuhimi wa kuwepo kwa mita hizo wakati wake umefika ili kuepukana na malalamiko kwa wateja wa kudai kubambikiwa bili za maji

“Ni kweli kupunguza malalamiko kwa wateja wetu kudai kubambikiwa bili za maji tumeona kufunga mita hizi za kulipia kabla ambazo tayari tumeshazifunga kwa wateja wetu wa majumbani pamoja na taasisi pia nifaida kwa taasisi na kuondoa malalamiko wateja “Amesema Masawe

Masawe amesema kwa muda kumekuwa na malalamiko kwa baadhi ya wateja ,pengine amepata bili anaona kama kunakubambikiwa na kadhalika ndiyo tukaona kuja na mita za kulipia kabla

Tulipo nyanyua wazo kuwa na mita hizi na Serikali ikaliuunga mkono imetusaidia kutafuta majawabu na kuanzia kama taasisi tumetoa maelekezo kwa shule tatu za ufundi ikiwamo ya Shule ya ufundi Arusha na nyingine ipo mkoani mbeya kuhakikisha zinadhalisha mita ambazo zinafaa kwa matumizi kwenye taasisi za maji Nchi nzima

Nashukuru Serikali imeunga mkono na imetoa maelekezo kwamba wakati sahihi sasa Wananchi kupata hii huduma bila malalamiko ,mtu anaweza kufahamu kwamba ametumia kiasi gani na jawabu ni hizi mita za kulipia

Amesema Wenzetu Tanesco wamefanikiwa sana,na sisi tunatamani kuiga kwa wenzetu wao wamefanikiwa kuweka Nchi nzima

Aidha Amesema katika mita hizi walizopokea na kuzifunga zipo changamoto zilizojitokeza kwa aina ya teknolojia iliyopo inatumia Sola ambayo inakuwa na Panel na Betr ambazo zimeweka sehemu ambazo mita zimefungwa

Amesema hivi karibuni wamepata changamoto kwa Wananchi wasio na nia njema kuiba zile Panel ,sijajua kwa matumizi gani,

Sasa ili nalo tumelijadili na tumewashirikisha waleotengeneza hizi mita kwamba aina ya teknolojia inaweze kuwa sio nzuri sana, nakuomba itengenezwe mita nyingine inayoweza kufanya kazi badala ya Sola ingefaa sana

Idrisa Mndeme Mkazi wa Sanya juu ,amepongeza utaratibu huo wa kulipia kabla , lakini ameomba mita hizo kuwekwa sehemu salama ambazo haziwezi kufikiwa na watu wenye nia mbaya ya kuziiba nakurudisha juhudi za Serikali za kuleta maendeleao

Mwisho