Site icon A24TV News

CCM Hai waonya ugawaji wa Aridhi kata ya kia

Na Mwandishi wa A24tv .

Chama cha mapinduzi (CCM), Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro kimeitaka ugwaji wa Aridhi katika Kijiji cha Sanya station kata ya KIA Wilayani hapo kuzingatiwe sheria na taratibu ili kuepusha malalamiko kutoka kwa Wananchi

Wananchi hao ni wale pamoja na vijiji vya Sanya station,Tindigani na chemka walioridhia kupisha eneo na kupewa fidia na Serikali baada ya kubainika kuwa kwenye eneo la Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa kilimanjaro (KIA).

Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya Wangub Maganda akiongea kwenye mkutano wa kuwasilisha na utekelezaji wa ilani ya CCM ya mwaka 2020,2023 kata ya KIA iliyofanyika katika Kijiji cha Sanya station kutoka kwa o,ametaka ugawaji wa Aridhi kuzingatiwa kanuni na Sheria

“Ni kweli nataka wausika kuzingatia utaratibu na Sheria katika kutoa aridhi ili kuepuka malalamiko na sintofahamu kutoka kwa wananchi”amesema Maganda

Maganda amesema nasikia wapo watu wanaotaka kuvuruga utaratibu mimi ukivuruga ugawaji wa Aridhi mkaleta tafrani ,kama tafrani iliyotokea hapa , Serikali imelipa sh,11 bilioni na point kwa sababu ya udhaifu wa Viongozi waliokuwepo hatutakubali”amesema Maganda.

Na nyinyi mnataka kuleta sintofahamu Naomba aridhi ya kia igawanywe kwa utaratibu wa kisheria na kulingana na mahitaji ya watu

Amesema Nasikia kuna matajiri wanataka kuchukua aridhi kubwa ,Kuna wengine wanataka eka 7 ,naomba rafikizangu kuweni makini ,mtendaji wa kijiji hiki kuwa makini

Kanuni na Sheria za aridhi ya kijiji namba 5 ya mwaka 1999 ,kwa bahati nzuri Sheria ile ni katika sheria chache za nchi hii zilizota tafsiriwa kwa kiswahili

Kwa hiyo naomba aridhi ya hapa ifuate utaratibu ,mimi tajitahidi kusema ukweli kona zote ili muradi watu wangu wasidhulumiwe

Joseph Laitayo Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Sanya station ,kwanza amemshukuru Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kumaliza mgogoro uliopo kata ya KIA ulidumu kwa muda mrefu zaidi ya miaka 30

Lakini watu wamepata haki zao na sasa hivi maisha yanaendelea ,tulikuwa na Aridhi ya Kijiji tunaendelea kuwapa watu kwa bei nafuu uko palestina na kitongoji cha Road toll lakini pia kuna Aridhi ipo eneo la darajani na pia tumetenga eneo la kujenga shule eka 12.

Amesema katika zoezi ilo la Aridhi walikuwa wanakwamishwa na watu wastaafu ambao hawana mema na Wananchi kutaka kuweka maslai yao mbele ambayo hayana maslai kwa Wananchi

Kwa hiyo zoezi bado kimaendelea kwa sababu kuna Wananchi bado wanaitaji Aridhi kwa sababu fidia ilikuwa inalipwa kwa awamu ilikuwa awamu ya mwisho

Tunashuru Mkuu wa Wilaya yetu Amiri Mkalipa pamoja na Mkuu wa mkoa Nurudin Babu tumeshirikiana nao sana blla kumsahau Mbunge wa jimbo hili Saashisha Mafuwe.

Pia tunashuru Diwini wa kata hii Tehera Mollel, kwa uwasilishaji na utekelezaji wa ilani ya CCM,amefanya mengi ndani ya kata ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa , nyumba za walimu,barabara zilizochongwa na josho la migugo

Mwisho