Na Geofrey Stephen ARUSHA
Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI(AFYA)Dkt Wilson Mahera amesema serikali ipo mbioni kuajiri watumishi wapya wa sekta hiyo ikiwa ni mpango mahususi wa kuboresha sekta ya afya nchini ili kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi hususani wahudumu ngazi ya jamii .
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ)yaliyolenga kuwajengea uwezo ngazi ya uongozi.
Alisema kupitia mpango huo mikoa kumi nchini,itanufaika na nyongeza ya watumishi wapya ukiwemo mkoa huo wa Tanga lengo ni kupunguza vifo vya mama na mtoto, kupunguza magonjwa ya mlipuko,maambukizi ya magonjwa yakiwemo Malaria.
Alitoa rai kwa wataalamu hao wa afya wanaopatiwa mafunzo, kutumia ujuzi huo wanaoupata kwenda kufundisha na wengine ili wakatoe huduma nzuri kwa wananchi huku wakizingatia maadili ya kazi yao.
Awali mkuu wa Taasisi ya CEDHA ,Dkt Johannes Lukumay aliipongeza serikali kupitia waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu kwa uwekezaji mkubwa wa zaidi ya sh, Trilioni 6.7 katika sekta ya Afya,uwezeshaji iliolenga kuimarisha miundo mbinu ikiwemo vifaa tiba ,dawa na kusomesha madaktari bingwa na bobezi.
Alisema mafunzo hayo yenye washiriki 53 kutoka mkoa wa Tanga yamelenga kuboresha huduma na utoaji wa mafunzo ya msingi ya menejimenti, uongozi na utawala ili kuziwezesha timu kusimamia,kuendesha na kuboresha huduma za afya,ustawi wa jamii na lishe katika ngazi ya Mkoa ,Halmashauri na ngazi za kutolea huduma za afya.
Dk Lukumay alisisitiza kuwa mafunzo hayo ,wataalamu hao wa afya watapata uelewabjuu ya stadi za uongozi na utawala na pia watafanya mtihani wa kuwapima (POST TEST) na taasisi hiyo ya CEDHA itawatunuku vyeti.
Katika hatua ngingine dkt Lukumay alisema pamoja na utoaji bora wa mafunzo hayo, Taasisi ya Cedha imekuwa na changamoto ya kupata idadi ndogo ya washiriki.
Alimwomba naibu katibu mkuu kusaidia kuhimiza wataalamu hao wa afya kuona umuhimu wa kuhudhulia mafunzo hayo muhimu katika mustakabali wa sekta ya afya nchini.
Naye mshiriki wa mafunzo hayo elekezi ya uongozi katika sekta ya Afya ,Dkt Steven Mwandambo mganga Mkuu Halmashauri ya jiji la Tanga,aliishukuru serikali kwa kuendelea kutatua changamoto katika sekta ya afya ikiwemo kuwapatia vitendea kazi yakiwemo magari.
Mafunzo hayo yamedhaminiwa na shiria la GIZ Kufanikisha mafunzo ayo ya viongozi wa afya kutoka Arusha na Tanga .
Ends..