Site icon A24TV News

EWURA YAWANOA WANAFUNZI WA FANI YA UMEME CHUO CHA UFUNDI ARUSHA ATC SASA KUFANYA KAZI KWA KUSAJILIWA

Na Geofrey Stephen Arusha .

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA),Mkoa wa Arusha,imewataka  wanafunzi wanaosoma kozi ya uhandisi  umeme, kuona umuhimu wa kuchukua leseni  inayotolewa na mamlaka hiyo ili kujiwekea mazingira mazuri na kulinda taaluma yao.

Akiongea na  waandishi wa habari wakati wa utoaji wa semina  kwa wanafunzi wa kozi ya uhandisi umeme inayotolewa na EWURA katika chuo cha Ufundi Arusha(ATC).

Lorivii Long’idu,Meneja EWURA kanda ya kaskazini akizungumza na vyombo vya habari juu ya elinu walio toa kwa wanafunzi wa chuo cha Atc Arusha 

Meneja wa EWURA kanda ya kaskazini, Mhandisi Lorivii Long’idu alisema lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha wanafunzi wa fani hiyo kutambua umuhimu wa kuwa na leseni pindi wanapohitimu masomo yao kwani ni kosa kisheria kufanya shughuli za ufundi umeme bila kuwa na leseni inayotolewa na EWURA.

“Jambo la kuwa na leseni ya ufundi sio geni mara kwa mara tumekuwa tukiwakumbusha wanafunzi wa vyuo umuhimu wa kuwa na leseni hasa katika mifumo ya ufungaji wa umeme “

Alisema kumekuwepo  na changamoto ya ufungaji wa mifumo ya umeme kwa watu wanaotumia vishoka bila kuzingatia viwango na kusababisha nyumba nyingi ama mitambo kuungua kutokana fundi aliyefunga kutokuwa na leseni ya taaluma hiyo na hivyo kusababisha hasara ya mali  ama kupoteza maisha.

Mhandisi Long’idu aliwashauri wananchi kutumia mafundi wenye leseni zinazotambuliwa na EWURA hali itakayosaidia kuondoa wimbi la vishoka wanaochafua taaluma ya umeme .

Aidha aliwataka wahitimu wa  kozi ya uhandisi Umeme kuchangamkia fursa tele za ufungaji mifumo ya umeme zilizoko kwenye miradi mkubwa ya umeme hapa nchini.

Eng. Seba Maginga ATC

 

Awali mwalimu mlezi wa taasisi ya uhandisi ATC, Mhandisi Seba Maginga alieleza umuhimu kwa wanafunzi kuwa na leseni itakayowatofautisha na vishoka wa mtaani ambao huvamia fani bila kuwa na taaluma ya ufundi.

Aliiomba EWURA kuendelea kutoa elimu hiyo kwa vyuo vingine nchini vinavyotoa kozi za kihandisi ili kuwasaidia wanafunzi kutambua umuhimu wa kuwa na leseni ya fani yao kwa gharama ndogo ya sh, 50,000.

Baadhi ya wanafunzi, Alex Nyava anayechukua shahada ya uhandisi umeme ,alisema mafunzo ya EWURA yamemfumbua macho kuona umuhimu wa kuwa na leseni itakayomsaidia kumlinda na kuwa huru  kufanya kazi sehemu yoyote .

Ends..