Site icon A24TV News

KILI FAIR YAFANA JIJINI ARUSHA MWAKA 2024 WATALII WAMWAGIKA VIWANJA WA VYA MAGEREZA MAWAZIRI BARA NA VISIWANI WAFIKA

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Angellah Kairuki, Amefungua Maonyesho ya Sita ya kili fair jijini Arusha akiwa ameambatana na  Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga. Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christin Makonda kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu- Kili Fair 2024 yanayofanyika kwenye viwanja vya Magereza Kisongo leo Juni 07, 2024.

Awali Waziri Kairuki amezindua maonesho hayo msimu wa tisa wa maonesho yalishirikisha zaidi ya makampuni 400 ya utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania, yakiwa na lengo la kuhamasisha Utalii Tanzania.

Karibu kutamazama picha katiko matukio mbali mbali .

Mkurugenzi wa kampuni ya Hanspoul Satbir Singh akizungumza na vyombo vy habari

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Visiwani Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi anatarajiwa kuzindua mradi wa kwanza wa uwekezaji katika visiwa vidogo vilivyoko Kisiwa cha Bawe tarehe 15 Juni mwaka huu 2024.

Kauli hiyo imetolewa leo Juni 07, 2024 na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Visiwani Zanzibar Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa onesho la Karibu Kili Fair 2024, akiwakaribisha washiriki wa onesho hilo kuhudhuria uzinduzi huo ikiwa ni mpango maalum wa kuvihuisha visiwa vidogo vinavyopatikana kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.

Mwaka 2021 serikali ya Zanzibar iliruhusu uwekezaji kwenye visiwa vidogo vilivyopo Unguja na Pemba ikiwa ni utekelezaji wa sera ya serikali ya kuimarisha uwekezaji kwenye sekta ya utalii na uchumi wa buluu ili kuongeza pato la Taifa.

Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yamezinduliwa leo Mjini Arusha na Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Angellah Kairuki aliyeambatana na Waziri wa utalii Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Hassan Abbas na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda na wageni wengine kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Katika hatua nyingine, Waziri Soraga amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Chrisrian Makonda kwa kutambulisha na kumuomba Rais Mwinyi kusaidia katika kuiunganisha Zanzibar na Arusha kiutalii, akisema mpango huo utasaidia katika kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo ya Utalii yenye kuingiza fedha nyingi za kigeni.

Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yamezinduliwa leo Mjini Arusha na Waziri wa maliasili na utalii Mhe. Angellah Kairuki aliyeambatana na Waziri wa utalii Zanzibar, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na utalii Dkt. Hassan Abbas na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe.Paul Christian Makonda na wageni wengine kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Matukio yakionyesha bidhaa bora katika banda la happy sausages ya jijini Arusha .