Site icon A24TV News

RASHIDI THOMAS JELA MIAKA 60 KWA KOSA LA KUBAKA NA KULAWITI MTOTO MDOGO

Hai,

Mkazi wa Kingereka Bomang’ombe Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro Rashidi Thomas (19),Dereva bajaji amehukumiwa kwenda kutumikia kifungo cha 60 jela kwa kosa la kubaka na kulawiti binti wa miaka (17 )ambeye ni mama lishe

Mwendesha mashitaka wa Serikali Lubulu Mbise mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi mwandamizi wa Mahakama hiyo Julieth Mawole , amesema kwamba tukio hilo june 19 mwaka jana.

Mwendesha mashitaka huyo ameeleza kuwa mshitakiwa siku ya tukio majira ya usiku mshitakiwa alifika sehemu wanapouza chakula na kumwambia huyu binti kwamba kuna mteja anahitaj chakula apelekewe

Hakufana hiyana kwa sababu ni jambo la kawaida kuwapelekea wateja chakula katika Maeneo yao ,binti alipima chakula na kumpeleka alikoagizwa lakini alipofika kwenye uchochoro karibu na Panone huyu kijana alimkaba na kumpeleka karibu na shule ya boma Sekondari na kufanyia ukatili huo

“Ni kweli alifika na kuagiza wali na kwamba aliyeagiza chakula hayupo eneo hili hivyo waongozane akachukue hela lakini walipofika kwenye uchocho alimkaba kwa nguvu na kwenda kufanyia kitendo hicho ambacho sio cha kiungwana”amesema Lubulu

Baada ya kitendo hicho alimtelekeza na kutimka ,ambapo binti huyu alikuja kusaidiwa na wapita njia na kurudisha sehemu wanapofanyia biashara ambapo mwajiri wake alichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwenye vyombo usika

Chisimba amesema kitendo alichofanya ni kinyume na kifungu namba 130 (1)(2)(e)na 131(2)cha Sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16 Kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022,

Kosa la pili kumuingilia kinyume na maumbile kinyume na kifungu 154(1)(a)na( 2) kilichofanyiwa marejeo 2022,,kesi hiyo ilikuwa na mashahidi 3 akiwamo muhanga mwenyewe, Daktar na mwajiri wake ,Adhabu hiyo anaitumikia kwa pamoja

Na pia kukithiri kwa vitendo hivyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hivyo mahakama inakuhukumu kwenda jela kutumikia kifungo cha maisha jela

“Ni kweli vitendo vya ubakaji na ulawiti vinazidi kuongeza ndani ya Wilaya yetu ili iwefundisho kwa wengine unakwenda kutumikia kifungo cha Miaka 60 jela”amesema Mawole

Mwisho