Site icon A24TV News

Waandishi kilimanjaro wapewa kongole kwa kuunga mkono juhudi za mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira

Na Bajati Moshi,

Serikali imewapongeza Klabu ya Waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro (MECKI) kwa kuona umuhimu wa kupanda miti Maeneo mbali mbali ikiwa pamoja na kwenye chanzo cha maji chemi chemi ya Miweleni ikiwa ni jitihada za kuonga mkono Serikali za mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira

Aidha imetaka Jamii pamoja na Wenyeviti wa vijiji pamoja na watendaji wa Maeneo hayo kuitunza miti hiyo ili iweze kukua na kufikiwa lengo lililokusudiwa.

Hayo yamesemwa na Senzia Msafiri Afisa Tarafa Moshi Magharibi,kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ,ambapo kimkoa yalifanyika katika chanzo cha maji Miweleni kwa zoezi la upandaji miti

” Kweli niwapo kongole kwa kuona umuhimu wa kupambana na uharibifu wa mazingira kwa kupanda miti maeneobali mbali huu ni uzalendo ,mmeenda sambamba na kauli mbio yenu inayosema waandisi wa habari na changamoto za mabadiliko ya tabia Nchi”Amesema Senzia.

Senzia Amesema nyinyi wenyewe ni mashahidi wa mkoa huo kiwango cha joto kipo juu sana tofauti na kipindi cha nyuma ,hiyo ina sababishwa na ukataji miti hovyo na uchomaji wa mkaa,

Amesema kama Serikali tukiona watu wenye taaluma mnajitolea kufanya shughuli Kama hii kwetu ni faraja sana ,tunawapongeza na wengine waiga jambo kama hili,tunza mazingira yakutunze mmefanya jukumu nzuri sana

Lisiwe ni zoezi ambalo mnalifanya na kuishia hapo,liwe zoezi endelevu,sisi jukumu letu ni kuitunza ,tunawasikuana na Wenyeviti wa vijiji na watendaji kuhakikisha hii miti inakuwa

Ramadhani Bingwa kutoka bodi ya maji Bondo la Pangani kitengo cha mazingira ,Amesema chanzo hicho chemi chemi ya Miwaleni kimepakana na vijiji vitatu tunaomba Viongozi wa Maeneo haya kulinda miti hiyo ili tija iweze kuonekana,

Alen Mshana Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisakisangeni pamoja na Nover Mgonja Mwenyekiti wa kitongoji ,wamesema watatekeleza na kuhakikisha miti hiyo inakuwa kwa kuzungushia uzui miti hiyo kwani maji ya chanzo hicho wanamifahisha watu wengi sana

Awali kwenye taarifa ya chama icho ilivyosemwa na Sia lymo ,kuhusu maadhimisho hayo,Amesema wamefanya zoezi la kupanda miti zaidi ya 500 katika Maeneo ya Kijiji cha Miwaleni Wilaya Moshi mkoani hapa Kama ishara ya maadhimisho hayo

Amesema Klabu katika kuendana na kauli mbio ya mwaka huu inayosema Waandishi wa habari na changamoto za mabadiko tabia Nchi, Klabu imetoa Miche ya miti 1000 katika shule ya Polisi Moshi (CCP),ikiwa ni sehemu ya za kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi

Mwisho