Site icon A24TV News

WANANCHI WILAYANI HAI MKOANI KILIMANJATO WAASWA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA

Hai,

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro Wangub Maganda ,ametaka Wananchi Wilayani humo kuanzia miaka 18 kujitokeza kwa wingi katika Maeneo yao muda utakapofika wa kujiorodhesha kwenye Daftar la wapiga kura ili wawe na sifa ya kupiga kura

Aidha amesema utakapofika wakati wa kupiga kura za maoni chagueni mtu ambaye atauzika ,anayekubalika na Jamii.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti huyo wakati wa mkutano mkuu wa CCM kata ya KIA wakati wa uwasilishaji utekelezaji wa ilani ya chama hicho mwaka 2020 na 2024 uliofanyika ofisi ya Kijiji cha Sanya Station , ambapo amesema ili uwe na sifa ya kuwa mpiga kura sharti unioredheshe katika Daftar hilo

Akizungumza kwenye mkutano huo Amewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiorodhesha muda utakapowadia ili kuwa na sifa ya kupiga kura

“Kwa faida ya CCM naomba mjiorodheshe kwenye Daftar la wapiga kura ili muwa na sifa ya kupiga kura na kuchagua Viongozi wazuri mnaowataka,kama hautajiorodhesha utakuwa hauna sifa hivyo itakuwa ni kazi bure “Amesema Maganda

Maganda amesema ombi langu ni kwamba ndugu zangu Wana kia jisajilini kwenye Daftar la wakazi ili tushindishe watu wetu ambao watakwenda kumbeba Samia Suluhuu Hassani na Mbunge wa jimbo hili Saashisha Mafuwe Kama jina lake litarudi

Aidha utakapofika muda wa kipindi cha kupiga kura za maoni,naombeni mpige kura mtu anayeuzika barabarani anayekubalika na Wananchi uko tunakokwenda kushindanisha na wenzetu

Amesema Msituletee mgombea ambeye abatengemea uhai wake kwa kuchanjwa chale za kiuno na Mganga wa kienyeji , msituletee mtu ambaye kazi yao ni kunyang’a nya watu Aridhi,mnakwenda kumsimamisha watu wanashangaa huyo naye ni mgombea amewapa mimba watoto wetu hapana

Hivyo naomba wana CCM wenzangu mamba mawili ,moja mkajisaliji ilikuwa na sifa ya kushiriki chaguzi zinazokuja ikiwamo ya Serikali za mitaa,pia wakati wa kura za maoni chagueni mtu ambaye atauzika ,

Amesema yupo kiongozi mmoja wa ccm amesema hivi msituletee wagombee ambao unatakiwa utembee na dodoki unamuombea kura uku unamsugua uchafu kwa sababu uso umejaa,sijui tunaelewana

Kwa upanda wake Siror Laitayo katibu wa CCM kata ya KIA,amesema watakekekeza ushauri wa Mwenyekiti wa CCM Wilayani hiyo,ambao unataka na kusisitiza umuhimu wa Wananchi kujiandikisha kwenye Daftar kwa ajili ya kupata Viongozi bora

Pia katika swala la kupata mgombea ambae Wananchi wanamtaka,amesema wamepanga kupata Viongozi hao watakaosaidia kuvusha ccm na kuweza kuwaletea meandeleo wananchi

Awali Diwani wa kata hiyo Tehera Mollel ,amesema walikuwa na Jambo la kuwasilisha utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya kata yake.

Taarifa ya kazi zilizoelekezwa katika kata ya kia kwa kipindi cha 2020 hadi December 2024 June ,kupitia ilani ya uchanguzi wa chama cha mapinduzi 2020 ,25

Kikubwa nilichukuwa naeleza ni kuhusu Miradi ambayo tayari imetekelezwa ,Miradi ambayo inafanya kazi ikiwamo ujenzi wa madarasa ambayo wanasomea, nyumba za walimu wanazoishi,

josho la mifugo tayari ,barabara zilizochongwa zimemalizika ,tunamshukuru Raisi Samia Suluhuu Hassani pamoja na Mbunge wa jimbo hili Saashisha Mafuwe kwa kutuletea fedha kwa ajili ya Miradi hiyo hatuna budi kutoa Shukrani

Mwisho