By A24 Tv
Mtaalii mmoja mwenye asili ya China amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya gari la Watalii lenye namba za usajili T603 DCL mali ya Kampuni ya Yonda Africa walilokuwa wanalitumia, kupata ajali likiwa njiani kurudi hotelini kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. Taarifa iliyotolewa usiku huu na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema “Majira ya saa 10 jioni July 28,2024 gari la Watalii lenye namba za usajili T603 DCL mali ya Kampuni ya Yonda Africa lilipata ajali likiwa njiani kurudi hotelini kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge katika Hifadhi ya Taifa Serengeti”
Gari hiyo ilikuwa na Watalii saba wenye asili ya China na Dereva Raia wa Tanzania, Mgeni mmoja alifariki dunia na wengine 6 walipata majeraha, mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mugumu na majeruhi sita wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali hiyo”
Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na Mamlaka nyingine ili kubaini chanzo cha ajali hiyo”