Site icon A24TV News

TANZANIA NI MAHALI SALAMA KIBAISHARA NA UWEKEZAJI 

Na Richard Mrusha

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele kutokana na mazingira ya uwekezaji kuboreshwa ,kumeifanya Tanzania kuwa mahali  salama pa kufanya biashara na uwekezaji.

Akizungumza leo Julai 3 ,2024 na waandishi wa habari katika banda la JKT kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ,Meja Jenerali Mabele amesema   hali hiyo imefanya watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini.

“Naipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira  mazuri ya kufanya biashara na hivyo watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa mahali sahihi pa kufanya biashara na uwekezaji.

Kuhusu ushiriki wao katika amaonesho hayo ,Meja Jenerali Mabele ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali la JKT  (SUMAJKT) amesema  wameshashiriki maonesho hayo mara nyingi na kwamba wamekuwa wakija na bidhaa bora ili wananchi wananchi waweze kununua.

Pia amesema SUMAJKT ina  kampuni bora ya ulinzi ambayo ni miongoni mwa kampuni bora za ulinzi na ni kampuni ya watanzania ambayo ina walinzi zaidi ya 16000 katika maeneo mbalimbali

“Kwa hiyo katika eneo hilo tu tumechangia kupunguza ombwe la ajira nchini ,pia tunayo kampuni ya usafi kwa sababu kama nilivyosema tunaangalia fursa,tumeona kuna fursa katika eneo hilo watanzania wanahitaji majiji,miji yao iwe safi lakini tunahitaji   vijana wa kitanzania ambao tumewaajiri na wapo katika kampuni ile ili kuwawezesha kutunza familia zao kwa hiyo niseme tu kwamba kampuni zetu tunazozianzisha kutokanana fursa tunazoziona na kwamba tunaweza kufanya biashara na kutoa huduma katika nchi yetu,”

“Maonesho haya sisi tunafanya biashara ambayo husaidia kuongeza uchumi wa nchi, na mwezi  wa sita mwaka huu ,tumeshiriki katika kutoa gawio kwa hiyo ni wachangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali, tunalipa kodi ,tena ni walipa kodi wazuri katika nchi yetu,hivi vifaa vyote  mnavyoviona hapa tunalipa kodi na hili ni jambo la msingi sana.

Kuhusu ushiriki wao wa  maonesho katika nchi nyingine amesema,wamekuwa wakishiriki maonesho hadi ya nje ya nchi na wameshaenda kwenye maonesho Commoro  ambapo wakati mwingine watu wa Comoro wanakuja kuzifuata Dar es Saaam .

Ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha  watanzania kufika katika banda la JKT kuona na kununua bidhaa zao kwani ni bidhaa hizo zina bora.

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena amesema JKT linekuwa likishiriki katika maonesho hayo na bidhaa mbalimbali ambazo vijana nao wanashiriki katika kuzitengeneza.

Amesema ushiriki wao katika maonesho hayo ni kuonesha namna ambavyo wamekuwa wakilea vijana wale wa kujitolea na wale wa mujibu wa sheria na kuwawezesha kujitegemea kiuchumi  pindi wanaponaliza mkataba wao JKT na kurejea mtaani .

“JKT limekuwa likifanya shughuli za uzalishaji mali katika Nyanja za kilimo , uvuvi na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali pamoja na shirika letu la uzalishaji mali (SUMAJKT),

“Kwa kuwa JKT limekuwa likichukua vijana wale wa kujitolea na wale wa mujibu wa sheria,pamoja na kufundishwa masomo ya ukakamavu ,uzalendo na hali ya kulipenda Taifa lao lakini vile vile wamekuwa wakifudishwa katika Nyanja za uzalishaji mali

‘Sasa katika eneo hilo vijana wamefundishwa kuzalisha bidhaa mbalimbali na kupitia vikosi na shirika lao.amesema

Mwisho