Site icon A24TV News

HOTEL YA PARROT JIJINI ARUSHA YAANZA KAZI RASMI BAADA YA MIAKA 20 YATOA AJIRA KWA WATANZANIA 500 WATALII KUANZA KUMIMINIKA, INAKUMBI ZA KISASA ZA MIKUTANO

Na Geofrey Stephen Arusha .
Mwenyekiti wa bodi ya Hoteli ya kitalii ya Parrot ya Jijini Arusha,  Abdallah Msele,amesema mradi huo wa hoteli hiyo umekamilika kwa 98% unatoa ajira rasmi 200 na zisizo rasmi 300
Ameyasema hayo leo kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa awali wa hoteli hiyo iliyopo barabara kuu ya col milditon kata ya kaloleni, kuwa uwekezaji wa Mradi huo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan  katika swala Zima la Utalii
Amesema Mradi huo ulianza mwaka 2004 ulikumbwa na changamoto na ulusimama hivyo mmiliki wake wa awali marehemu,Abdallah Idd Mshana,aliomba mikopo benki ya Uwekezaji na mitaji TIB,iliyotoa mikopo uliowezeshabujenzi kuendelea.
Msele,amesema kuwa hoteli hiyo itakuwa na Vyumba 116,migahawa mitatu na kumbi 9 za mikutano.
Ameomba mifumo kati ya mamlaka ya mapato nchini TRA na Kituo cha uwekezaji TIC uwe inasomana Ili kuwaondolea usumbufu Wawekezaji wa miradi mikubwa  .
Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo,amepongeza uwekezaji wa Mradi huo mkubwa  uliofanywa na wazawa na kuwa ni kielekezo kizuri.
Amesema changamoto zilizopo zitaendelea kufanyiwa kazi ili kuendelea kutoa unafuu kwa wawekezaji wa miradi mbalimbali nchini.
Kwa upande wake  meneja wa benki ya Uwekezaji TIB,Samweli Michael Minja,amesema wametoa ufadhili wa Mradi huo ili kusaidia kukamilisha Mradi  huo unaotekelezwa na wazawa.
Mwisho.