Site icon A24TV News

KARIAKOO FESTIVAL KUWAUNGANISHA WAFABISHARA ZAIDI YA ELFU THELATHINI NA TANO

Na Richard Mrusha

JUMUIYA ya wafanyabishara wa Kariakoo leo imetambulisha rasmi tamasha la Kariakoo ilijulikayo kama ‘Kariakoo Festival’ litakalowakutanisha wafanyabishara wakubwa na wadogo ili kuuza bidhaa zao kwa bei ya punguzo na kuwaunganisha na wateja wa ndani na nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa kutambulisha Kariakoo Festival,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo,Martin Mbwana amesema tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Agosti 24 hadi 31,2024 katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo la tamasha hilo ni kumuunga mkono Rais Samia kwa kauli yake kuwa Kariakoo inaweza kuchangia kipato kikubwa kwenye serikali na kutangaza wafanyabiashara kwasababu kumekuwa na changamoto kubwa ya wafanyabishara wanakuwa na mizigo ya hadi miaka mitatu au minne kwenye stoo na magodown hivyo wameshirikaana na serikali na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwenye hilo soko ambalo watauza kila kitu.

“Lengo lingine ni kujitangaza wanauza bidhaa gani na wanapatikana wapi tunataka kufuangua karikakoo kwa nchi nane ambazo zinatuzunguka na hii ni historia kubwa katika nchi leo tumeanza tumewashauri wafanyabishara hata wa nje ya Kariakoo na mikoa mingine wajisajili kwenye kanzi data yetu na baada ya kusajili tutaangali namna TRA itatuwekea mazingira ya kuuza mizigo.

Mbwana ameeleza kuwa wameshirikisha watu wote na biashara za aina zote kama watu wa mizigo,mama ntilie na wanatoa elimu kwanza kwa wafanyabishara hao.

“Hii ni mara ya kwanza watajifunza vingi na tutafanya hivi kila mwaka mwitikio ni mkubwa na wafanyabishara wanapenda mabadiko na idadi ya wafanyabiashara kariakoo ni 35,000 hadi 40,000 tunategemea kupate wafanyabisha 15000 hadi 20000 ,”amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya One Voice na Mbunifu wa Tamasha la kwanza la Kariakoo Festival, George Lupenza amesema kwa siku ya kwanza na pili watakwenda kutangaza bidhaa zinazouzwa kwa bei ya punguzo na siku inayofata ni siku ya bidhaa za viwandani na baada ya hapo kutakuwa na bidhaa za nyumba na siku inayofuata biashara ya nguo.

“Tutakuwa na siku ya bidhaa za watoto na siku ya bidhaa zote za wanawake zitauzwa na tunategemea kuwa na wasanii wa ndani na nje na watu watazungumza mambo yanayowahusu.

Ameongeza “Niwashukuru jumuiya kupokea wazo hili na hii ni sehemu ya kuwakutanisha pamoja kuuza na kutangaza bishara zao kwani kariakoo inakusanya mataifa tisa Afrika na uchumi wan chi zingine unategemea karikakoo na mtu yoyote aliye na malengo anakuja na kuanza biashara na kufanikiwa haijalishi elimu aliyonayo vijana wamejiajiri na kubadilisha uchumi wao.

Naye Balozi wa kutangaza Kariakoo Festival ,Clara Damford amesema wafanyabiashara wakubwa na wadogo watawakutanisha na wateja kwani kariakoo ni kitovu cha biashara na watawapa fursa ya kupata masoko mapya na kupata mauzo ya bidhaa ambazo zimekaa stoo muda mrefu watauza kwa bei punguzo .

“Tutatatua migogoro ya wafanyabiashara iliyopo kwasababu tutawakutanisha na wadau kama Brela,TRA na wengine na litaunga mkono juhudi za matumizi ya nishati safi na mbadala ya kupikia na tumeandaa mashindano ya wanawake kwenye kupika kwa kutumia nishati safi,”amesisitiza Clara.

 

Mwishoo……