Site icon A24TV News

MZEE WA MIAKA92 AJENGA MAJENGO MATATU YA KISASA AMTAJA RAIS SAMIA,DC KAGANDA. ATOA ZAWADI NZITO KWAKWE

Na Geofrey Stephen Arumeru

Mkuu wa wilaya EMMANUELA MTATIFIKOLO KAGANDA amepokea Majengo matatu ya kisasa kutoka kwa Mdau wa Maendeleo Mzee Aminiel Nko. kikongwe wa miaka 92 mkazi wa seela Sigisi Wilayari Arumeru Mkoani Arusha .

Akipokea majengo hayo kwa niaba ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan Kaganda amewataka vijana kuiga mfano mzuri wa uzalendo alioonyesha mzee huyo kwa kujali jamii yake inayo mzunguka kwa kujenge ofisi Kituo cha Polisi, kilicho jengwa kwa gharama ya Milioni 60, Ofisi ya Kijiji milioni 50 na ya CCM milioni 50 ambazo zote kwa pamoja zimezinduliwa tayari kwa matumizi ya wanachi wa kata hiyo na kata za jirani.

Kaganda amesema kwamba licha ya mzee Aminiel  kuonyesha uzalendo wa kujitolea ujenzi wa ofisi hizo pia ni mtazania ambaye anapenda viongozi akiwemo hayati Mwalimu Nyerere , na sasa mahaba yake yapo kwa Mh Rais Samia kwa uchapaji wake mzuri wa kazi kwa watanzania .

Awali Mzee Aminiel Nko Maarufu kwa Jina la Mzee korii akikabidhi miradi hiyo kwa mkuu wa wilaya amesema kwamba amependezwa kujenga majengo hayo kwa lengo la kusaidia wananchi wenzake kupata huduma kwa uraisi na kuondoa changamoto ya kufuata huduma mbali ya kijiji chake  na anaunga mkono jitiada za kazi zinazo fanywa na Mh Rasi ya awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan.

Mwisho.