Site icon A24TV News

KIONGOZI WA MWENGE KITAIFA AWATA WALIMU ARUSHA KUWASIMAMIA WANAFUNZI KULINDA MIUNDO MBINU YA SHULE

Arusha

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2024, Godfrey Eliakimu Mnzava amewataka walimu kusimamia wanafunzi wao kutunza miundombinu ya shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha iliyoko kata ya Olasiti jijini Arusha.

Amesema kufanya hivyo kutasaidia miundombinu ya shule hiyo kudumu kwa mda mrefu na kuwanufaisha wanafunzi waliopo sasa na vizazi vijavyo.

Mnzava ameyasema hayo leo Julai 22,2024 wakati akizindua mradi wa ujenzi wa vyumba 15 madarasa, mabweni 2 na matundu 21 ya vyoo 21 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Arusha iliyoko kata ya Olasiti.

Mradi huo uliotekelezwa na serikali kupitia Kampuni ya madini Barrick kwa gharama ya shilingi milioni 679.1 umetembelewa na kukaguliwa Leo na msafara wa mwenge wa Uhuru ambapo kiongozi wa msafara huo akisindikizwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha Juma Hamsini ameridhishwa bila kuacha shaka na mradi huo.

 

Baada ya Ukaguzi Mnzava amesema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira rafiki ya wadau kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Na lengo kubwa ni kusogeza huduma kwa wananchi na kuweza kunufaika na uwekezaji huu, hivyo basi haitapendeza wanafunzi waliopo mruhusu waharibu Ili baadae vizazi vijavyo wakose huduma hii njema” amesema Mnzava.

Mbali na hilo aliishukuru Kampuni ya Barrik kwa kurudisha huduma kwa jamii.

“Tunaishukuru Kampuni ya Barrick kwa mchango wake mkubwa kwa jamii, serikali inatambua na kuthamini kazi hii kubwa na ya kizalendo iliyofanywa, inayowezesha watoto wa kitanzania kupata elimu kwenye mazingira rafiki” .

Mwisho…