Site icon A24TV News

KISHINDO CHA MAIPAC KWA MARA YA PILI YAZINDUA MRADI KUSAIDIA UIFADHI WA MAZINGIRA KWA WILAYA MBILI MKOANI ARUSHA

Na Geofrey Stephen Mto wa Mbu
Kwa mara ya pili tena kwa kishindo kizito Taasisi ya wanahabari ya usaidizi wa Jamii za Pembezoni (MAIPAC) imezindua mradi wa uhifadhi wa mazingira kwa kutumia maarifa ya asili huku Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli ameahidi kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kituo Cha kujifunza maarifa ya asili Mradi huo wa Mazingira unafadhiliwa na Mfuko wa Mazingira Duniani(GEF) kupitia program ya miradi midogo ambayo inasimamiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) na kuratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli mkoa wa Arusha, Isack Joseph amezindua mradi huo leo, Julai 6, 2024, katika hafla iliyofanyika hoteli ya Makambo te makuti iliyopo Kigongoni mto wa Mbu wilaya ya Monduli Mkoani Arusha. Joseph akizungumza katika uzinduzi huo aliipongeza taasisi ya wanahabari ya MAIPAC
kwa kubuni mradi huo ambao unasaidia vita dhidi ya athari za mabadiliko ya Tabia nchi. “Nawapongeza MAIPAC kwa kuja na mradi
huu kwanza kujenga uzio katika chanzo cha maji cha Kabambe kata ya Selela lakini pia atika eneo la Eyasi kwenda kukusanya
“Nawapongeza MAIPAC kwa kuja na mradi huu kwanza kujenga uzio katika chanzo cha maji cha Kabambe kata ya Selela lakini pia katika eneo la Eyasi kwenda kukusanya maarifa ya asili katika uhifadhi”alisema.
Mwenyekiti huyo, alisema halmashauri hiyo ipo tayari kutoa ardhi kwa ajili ya ujenzì wa kituo cha kuhifadhi maarifa ya asili ambapo watu watakuja kujifunza Mila,Tamaduni na maisha ya jamii za asili.
‘Nimesikia maombi ya Mkurugenzi wa MAIPAC
Mussa Juma kuomba ardhi kwa ajili ya ujenzi
wa kituo cha maarifa ya asili sisi tupo tayari
<utoa ardhi tunaomba kuletewa barua rasmi ya
maombi”alisema.
Awali Mkurugenzi wa MAIPAC ,Mussa Juma
alisema mradi huo unatekelezwa kwa awamu
ya pili awamu ya kwanza ilikuwa wilaya za
Longido, Ngorongoro na Monduli na Sasa ni
wilaya mbili za Karatu na Monduli .
Alisema lengo la mradi huo ni kusaidia
uhifadhi wa mazingira, vyanzo vya maji na
Misitu kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo
Tumebaini Kuna maarifa mengi ya asili ya19:00
uhifadhi mazingira hivyo MAIPAC tunakwenda
kuyakusanya katika nakala ngumu na laini na
baadae kutengeneza kitabu kwa awamu ya pili
“alisema.
Juma alishukuru GEF,UNDP na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira kuendelea kutoa fedha kwa MAIPAC ili itekeleze miradi ya mazingira na kutunza vyanzo vya maji.
Akizungumza Kituo Cha kutunza maarifa ya
asili alisema wanaomba kupatiwa ardhi ili
kuanza mikakati ya ujenzi wa kituo ambacho
pia kitakuwa kitega uchumi kwa jamii za
pembezoni,

Awali Afisa Misitu wilaya ya Karatu, Reginald Hallu alisema wilaya hiyo kama wilaya nyingine zinakabiliwa na changamoto ya uharibifu na mazingira hasa kwa wananchi kulima katika vyanzo vya maji..

Hallu alisema halmashauri imekuwa  ikichukuwa hatua mbalimbali Kudhibiti na akapongeza MAIPAC kuungana na serikali na kupeleka mradi wa mazingira lake Eyasi..

Naye Afisa misitu tarafa ya Manyara, Happy Masaki alisema mwaka juzi MAIPAC ilikuwa na mradi wa mazingira katika kata ya Selela na aliomba wajengewe uzio katika chanzo Cha maji Kabambe na anashukuru MAIPAC kukubali na mwaka huu wanajenga.

Wakizungumza katika uzinduzi huo wananchi wa Selela na Eyasi walipongeza MAIPAC kuja na mradi huo na kuahidi wataendelea kutoa ushirikiano.

Halima Mollel mkazi wa Selela alisema wanaipongeza Taasisi ya wanahabari ya MAIPAC kurudi katika kata ya Selala kutekeleza mradi wa ujenzi wa uzio katika  chanzo cha maji Kabambe..

Afisa miradi wa Shirika la Jumuiko la Maliasili Tanzania (TNRF) Stevin Ngowi na Mkurugenzi wa Shirika la MPDO ,Lebaraka Laizer ambao mashirika Yao yanafadhiliwa na UNDP pia walieleza MAIPAC limekuwa Shirika la mfano kwa kutekeleza vyema. miradi.

Ngowi aliomba halmashauri ya Karatu na wananchi wa Eyasi kushirikiana vizuri na MAIPAC kama ilivyokuwa wilaya za Longido , Ngorongoro na