Site icon A24TV News

MARANYA AVUMBUA KIFAA CHA KUFUNDISHIA MFUMO WA JUA

Na Richard Mrusha

MBUNIFU wa mradi wa kifaa cha kufundishia Mfumo wa Jua, Sayansi ya Anga na Muundo wa Atomu Ernest Maranya amesema kuwa kupitia Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),amebuni kifaa hicho kwa lengo la kufundishia shule za msingi na sekondari nchini.

Akizungumza leo Julai Mosi jijini Dar es Salaam kwenye maonesho ya 48 ya kimataifa ya Biashara Dar es Salaam (DITF), amesema kuwa mradi huo umekamilika ambapo umetolewa mtaala na kuruhusiwa uweze kutumia kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Mbunifu huyo ameongeza kuwa mradi huo umepitia hatua mbalimbali za tathimini katika mamlaka zinazohusika na elimu ikiwamo Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Amesema kifaa hicho kimelenga kufundishia wanafunzi wa elimu za msingi na sekondari lengo likiwa ni wanafunzi hao kujifunza kwa njia ya ulahisi.

” Baada ya kufanyiwa mchakato wa kutathiminiwa serikali imeweza kuidhinisha kifaa cha kufundishia kama mitaala kwa ajili ya kufundishia wanafunzi hivyo tumekileta kifaa hiki hapa kwenye maonesho ili kuionesha jamii na wadau wa elimu,” ameeleza.

Ameeleza kuwa kupitia VETA amebuni mashine mbalimbali ikiwa ni pamoja na kifaa hicho huku akisema lengo la ubunifu huo ni kusaidia mahitaji mbalimbali ya jamii kama uchakataji wa mazao kutengeneza mashine ya kusaga karanga, kahawa na mazao mengine.

Mbunifu huyo ameishukuru serikali pamoja na VETA ,Tume Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kwa ushirikiano ambapo wameweza kufikia hatua hiyo huku akisema manufaa ya kifaa hicho ni makubwa katika sekta ya elimu.

MWISHO