Site icon A24TV News

MAZIKU AIANGUKIA SERIKALI KUBORESHA USIKIVU

Na Richard Mrusha

MWALIMU wa Chuo cha VETA Kigoma Innocent Maziku ameiomba Serikali kupitia watafiti wake kutoka Wizara ya Afya kukifanyia utafiti kifaa cha kuboresha usikivu kwa watu wenye usikivu hafifu ili azalishe vifaa hivyo kwa wingi zaidi ili vigawiwe shuleni kwa watoto wenye changamoto hiyo.

Akizungumza kwenye banda la VETA jijini Dar es Salaam kwenye .aoneaho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara Maziku amesema kifaa hicho alichoanza kukibuni oktoba mwaka jana,kimekamilika tangu Machi mwaka huu lakini anashindwa kuendelea kuvizalisha kwa wingi kwani bado hakifanyiwa utafiti wa kujua kama kina madhara ya kiafya kwa mtumiaji.

Amesema kuna Idadi kibwa ya vijana wenye usikivu hafifu wamefika kwenye VETA na kukijaribu kifaa hicho na kuonekana kina tija ila changamoto yake ni kwamba bado hakijafanyiwa huo utafiti.

Kwa mujibu wa Maziku pindi uzalishaji utakapoanza kufanyika kwa wingi ,itasaidia wazazi na wananchi kwa ujumla wenye watoto wenye changamoto hiyo kumudu gharama ya kifaa hicho ambayo ni ndogo tofauti na kinachouzwa hospitali ambacho gharama yake ni zaidi ya shilingi 1.5 milioni .

“Utengenezaji wa hiki kifaa unatumia gharama ndogo sana ,kwa hiyo ponsi kitakapoanza kuzalishwa kwa wingi watu wengi wataweza kumudu gharama kwa watu wa kawaida ila kwa wanafunzi VETA Kigoma itagawa bure kuwawezesha kuwa na usikivu mzuri darasani.”amesema Maziku

Maziku ambaye anatumia kwa ajili ya usikivu kifaa alichokitengeneza mwenyewe amesema ,kwa sasa kifaa hicho kinamsaidia kuboresha usikivu wake anapoongea na watu ingawa bado hakipo rasmi.

Xxxxx