Site icon A24TV News

MFUGAJI WA NGAMIA WILAYANI HAI AMZAWADIA RAIS SAMIA NGAMIA

Na Bahati Hai .

mfugaji wa Ngamia Kijiji cha mtakuja Wilayani Hai mkoani Kilimanja ameahidi kumpatia Rais Samia Suluhuu Hassani Ngamia.

Serikali imeombwa kuhamasisha jamii kuhusu ufugaji wa Ngamia na faida zake ili iweze kuwa na mwamko wa kufuga na kupata maziwa pamoja nyama kwani itasaidia kuinua kipato cha familia

Akizungumza na waandishi wa habari leo mfugaji wa wanyama hao Dahir Jama Yussuf mkazi wa kijiji cha Mtakuja kata ya Kia, wilayani Hai mkoani waliomtembelea kijijini hapo, kufahamu namna alivyo weza kuwafuga wanyama hao amesema wanafaida kubwa

“Ni kweli wanafaida kubwa ndiyo sababu naomba Serikali iweke kipaumbele kuhamasisha jamii kufuga Wanyama hao,baadhi katika Kijiji hiki wameaanza kufuga na faida wameaanza kuona ‘amesema Dahir.

Akizungumzia kuhusu maziwa hayo yametajwa kuwa moja ya chakula muhimu chenye virutubisho vingi vyenye kinga ya magonjwa mbalimbali mwilini yakiwemo magonjwa ya, kisukari vidonda vya tumbo, pumu, upungufu wa vitamin C alisema

Na kwamba ngamia mmoja anauwezo wa kutoa lita ishirini kwa siku moja na maziwa lita moja inauzwa sh,3000,,ambapo alisema soko lipo baadhi ya mikoa kilimanjaro, Arusha ,Dodoma na Daar salaam hadi nje ya Nchi na kwamba Ngamia mmoja mkubwa anauzwa sh,2,0000

Dahir amesema Changamoto kwamba baadhi ya watu wanamuamko mdogo kuhusu unywaji wa maziwa hayo hivyo kusababisha soko kuwa dogo la bidhaa hiyo na kwamba ufugaji huo ameanza toka 1990 na sasa ana ngamia 96

Alisema mbali na kuwa na faida hiyo ya kutoa maziwa yenye virutubisho ,ngamia ni mnyama anayeweza kutumika kubebea mazao shambani , usafiri wa kubebea wagonjwa au kama usafiri wa kawaida kutoka eneo moja hadi jingine.

Hivyo kushauri kama alivyosema awali jamii ihamasike kufuga Wanyama hao wenye faida kedekede ili kujiongezea kipato cha familia na Taifa kwa ujumla

Mbali na hilo amempongeza Rais Samia Suluhuu Hassani kwa kuleta maendeleao kwenye kata hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa fedha Sekondari eneo la tambarare,kujenga chuo cha veta na ujenzi wa kituo cha Afya

Kutokana na kukoshwa na maendeleao hayo ameahidi kumpa Ngamia mbili au tatu kumpongeza Mama Samia Suluhuu Hassani kutokana na jitihada hizo atakapofika katika eneo hilo

Tehera Mollel amepongeza mwananchi huyo kwa kuanzia Mradi huo wa ufugaji na kwamba vijana zaidi ya kumi wamaajiriwa kutunza mifugo hiyo

Kwa upande wake Mkurungenzi wa Kituo cha utafiti wa Mifugo Kilichopo Westi Kilimanjaro Wilayani Siha, Leonard Marwa,alisema maziwa ya Ngamia ni mazuri sana

Amesema kimsingi ni kwamba maziwa tunavyosikia ni dawa inaambatana na chakula anachukula,kuna jamii ya mimea ,jamii hiyo ya mimea inasababisha yale maziwa ionekane kwamba ni tiba

Kwa hiyo kama atabadilishiwa mazingira ale chakula cha tofauti kabisa hiyo nguvu ya haya maziwa kuwa tiba lazima itashuka

Kwa hiyo kinacho amua ndiyo hicho mwili huo sasa hauwezi kuzalisha kemikali itakayo tibu jambo flani ,hii inayotibu inatokana na mimea

Mwisho