Site icon A24TV News

moto wateketeza vyamba 11 vya wapangaji Ngarenairobi Wilayani Siha

Siha,

Nyumba yenye vyumba 11 vya wapangaji Kijiji cha Ngarenairobi Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro iliyojengwa kwa mbao vimeteketea kwa Moto na kusababisha hasara kubwa

Tukio hilo kulitokea julai 6 mwaka huu majira ya saa moja na nusu usiku, chanzo kikidaiwa kuwa na jiko la ges kulipuka kwenye mmoja ya chumba cha wapangaji,

Ambapo pia Wananchi wakishauriwa kujenga nyumba za kudumu kwa kutumia tofali.

Mtendaji wa Kijiji hicho Seif Mwemgamba Akizungumza na waandishi wa habari ,amesema moto huo, umesababisha hasara kubwa ambapo ,umeteketeza kila kilichokuwa ndani ya nyumba

“Yaani mtu alivyotoka ndivyo hivyo alivyo ,kama nguo alizovaa ndivyo hizohizo vitu vyote vimepungua ikiwamo ,vitanda,Magodoro ,tv,pikipiki mpya king lion pia imeungua,thamani ya vitu bado haijajulikana”amesema Seifu

Seifu anasema kutokana na janga hili la moto kutokea Mara kwa mara katika eneo hilo hasa kwenye nyumba hizi zilizojengwa kwa mbao na kuwasabishia hasara kubwa kwa Wananchi, wameshauri kujenga nyumba za kudumu kwa kutumia tofali

Akitolea mfano amesema hapo Ngarenairobi tena mwezi haujaisha nathani wiki mbili nyumba moja iliungua na vitu kuteketea ,kama Viongozi niwajibu wetu kutoa ushauri alisisitiza Seifu na Matadi kata ya Indumet nyumba mbili zikiungua na vitu kuteketea hii ni hasara na inarudisha juhudi za maendeleao nyuma

Kutokana na hilo, yaani tunachukifanya ni kujaribu kuwahamasisha Wananchi kujenga nyumba za tofali za kudumu,hata kama unakipato kidogo usijenge kubwa

Anza na chumba kimoja viwili polepole ukienda shambani ukivuna kidogo unasongeza hivyo mpaka miaka 4 au 5 ,nyumba itakuwa imekamilika

Amesema hata jana hii nyumba iliyokuwa inapungua kuna upande wa mashariki na kusini kuna ukuta wa uliojengwa kwa zege ,huu ndiyo umenusuru nyumba nyingine zisishike motonimuhimu wataalamu kutoa elimu. Kuhusiana na namna ya kuepukana na majanga ya moto

Kwa upande wake Robart Mrisho yeye ameshauri kwamba njia Moja wapo ya kuepukana na majanga ya marakwa mara ni pamoja na kujenga nyumba na kuweka umbali kati ya nyumba Moja na nyingine

Mirisho amemuomba Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka pamoja na wataalamu wa mipango miji na kufanya ziara kwenye kata ya Ndumeti na Ngarenairobi Moja ya sababu ya msongamano wa makazi ktk kata hizo

Mkuu wa Wilaya hiyo Christopher Timbuka,amekiri kutokea kwa tukio hilo,ambapo amesema moja wapo ni kutaka kuwatafutia makazi ,hiyo utafanyika ,hii itakamilisha ,kingine tahadhari , ukiangalia matukio mengi yametokea kule na kwa sasa naelekea uko

Mwisho