Site icon A24TV News

MWENGE WA UHURU WAZINDUA MIRADI MBALI MBALI WILAYANI ARUMERU ZIKIWA KWENYE UBORA MKUBWA

Na Geofrey Stephen Arusha

Kanisa Katholiki kupitia Kituo cha Malezi ya watoto cha St. Mary’s Children’s, imefuraishwa na kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayotoa huduma kwa jamii chini huku Serikali ikithamini mchango wa kanisa hilo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu, Godfrey Eliakimu Mnzava,  kabla ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Kituo hicho, kilichojengwa na Kanisa wenye thamani ya shilingi milioni 950, kilichopo kata ya Kikwe Halmashauri ya Meru wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha  leo Julai 19, 2024.

Kiongozi huyo Amesema kuwa, licha ya Kanisa hilo kutoa huduma za kiroho kwa karne kadhaa sasa lakini limekwenda mbele zaidi katika kutoa huduma kwa jamii katika seka za afya, elimu na kutekeleza miradi mingi kwa kuwa na Programa mbalimbali na endelevu za kutoa msaada kwa watu wenye uhitaji na majitaji maalum.

Kiongozi wa Mwenge wa Uburu Mnzava wakati akiweka  jiwe la Msingi, amepongeza ujenzi wa Kituo hicho cha Kulelea watoto wenye mahitaji Maalum  na kusema kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango wa kanisa hilo katika kutoa huduma kwa jamii ambazo kimsingi lilikuwa ni jukumunla Serikali.

 

 

katika uwekaji wa jiwe la msingi kiongozi wa mbio za mwenge ametumia wasaa huo kutoa Jumbe za Kidumu za Mwenge wa Uhuru, ikiwemo mapambano dhidi ya ugonjwa wa Malari, matumizi ya Dawa za Kulevya, VVU – UKIMWI sambamba na kuhamasisha wananchi kuzingatia Lishe Bora pamoja na kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kujiandikisha kwenye daftari la Wapiga kura.

 

Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru 2024 ni “Tunza Mazingira, Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu”

 

Mwisho .