Na Richard Mrusha
Taasisi ya Udhibiti wa shughuli zote za utafutaji uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi nchini (PURA) waja na mpango mkakati wa kujenga mazingira bora yanayovutia kwa wawekezaji wa sekta ya mafuta na gesi wanaokuja kufanya utafiti na uwekezaji nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Petroleum Upstream Regulatory Authority ( PURA ) Mhandisi Charles Sangweni ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitembelea maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba 2024) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Amesema wanatarajia kutangaza maeneo watakayowashawishi na kuwavutia wawekezaji kuwekeza katika Sekta ya Mafuta na Gesi kwa yale maeneo huru ambayo hayamilikiwi na nchi yoyote, na pia tayari wameisha pata vibali kutoka umoja wa mataifa.
Mhandisi Sagweni Amesema maeneo hayo wameyagawa katika vitaru ukanda wa Pwani ndio watakao anzia kutangaza kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji kuja kuwekeza,lakini pia ndio maeneo yaliyogundulika kwa gesi inayotumika sasa.
Amesema mpango wao ni kuendelea kutangaza vitaru hivyo kwa awamu na wanatarajia kueneza nchi nzima kama vile Singida,Manyara, na Tabora,maeneo ya ziwa Tanganyika kama vile Kigoma, na Maeneo ya kusini.
Amesema katika mnyororo wa kuongeza thamani ya Petrol wana mikondo mitatu,ambayo ni Mkondo wa Juu unaohusu kutafuta,kuendeleza,na kuzalisha Petrol,Mkondo wa kati ambao baada ya ugunduzi wa maeneo yenye uwepo wa mafuta ambayo huwa katika mfumo wa tope hivyo husafishwa na kuchakatwa kuweza kupata Petrol,Disel na Mafuta ya taa.
Amesema mkondo wa tatu ni mkondo wa chini ambao sasa haya mafuta huuzwa,baada ya kusafiriswa.
Mwisho…