Site icon A24TV News

Rc Kilimanjaro atoa mwezi mmoja halmshauri kukusanya mikopo waliotoa kwa vikundi na kushindwa kurejesha

Na Bahati Hai.

Siha,Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu ametoa siku 30 kwa halmshauri za mkoa huu kufutilia na kurejesha mikopo ya asilimia 10 ambavyo vikundi vilikuposhwa na halmshauri hizo na kushindwa kurejesha

Kauli hiyo ameitoa leo katika kikao maalumu Baraza la madiwani kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG)kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri,nakuhudhuriwa na Viongozi wa Dni , Madiwani ,wakuu wa idara

Akizungumza katika kikao hicho ametoa mwezi mmoja kwa anayedaiwa kurejesha fedha hizo ili na wengine waweze kukopeshwa

” Sasa natoa agizo nawala sio ombi kote nilikopita nimetoa mwezi mmoja kuhakikisha fedha zote zinakusanywa na hawa walizopewa mikopo wanajulikana na waheshimiwa Madiwani mnawajua wengine wanatoka kwenye kata zenu,kwa nini wanaofanya hivyo

Babu amesema ,ingekuwa wamechukua fedha Bank ,Bank si mnajua msingefanya mchezo kama huu,sasa hivi wangesha uza nyumba ,gar,wangeuza kila kitu.

Kwa hiyo Mkurungenzi mtendaji wa halmshauri pamoja na Mwenyekiti wa halmshauri ndani ya mwezi fedha ziwe zimekusanywa,
Kuna sh,15 milion na sh,83 milion ziwe zimekusanywa na

Amesema katika taarifa ya maandishi ili tunapokwenda kwenye bajeti Mungu akituweka hai nataka kuwa umenisainia kwamba mikopo imerudi ili sasa vijana wengine,wanawake na walemavu waweze kupewa hizi fedha.

Amesema ,nyie Siha mpo kwenye zile Wilaya 10 za kupewa mikopo , sasa hawatatuchezea tena fedha watakazo pewa zitalipiwa bank

Pia ameomba wakurungenzi watendaji wa halmshauri kuhakikisha shule za Msingi na Sekondari mkoani hapa zinapatiwe hati miliki,Mimi nimeshasema sana nashangaa,Sasa natoa maelekezo Wakurngenzi na timu zenu ,shule zote za Sekondari na msingi ziwe na hati haraka iwezekanavyo

Aidha kitu kingine ametaka halmshauri hiyo ipunguze hoja zisiwe zaidi ya mbili wakati mwingine ,lakini kwa nini tuwakuwa na hizi hoja ,nataka wa idara wote mshiriki kikamilifu katika swala nzima kuzuia kuwepo kwa hoja,nyinyi wakuu wa idara tunategea muwasaidia madiwani

Sambamba na hilo ameipongeza halmshauri kwa ukusanyaji mapato ,nitakuwa mchoyo wa fadhila mmefanya vizuri sana June 30 mwaka huu mmefikia asilimia 110 niwapongenze sana mnatubeba.

Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancani Urasa,Amesema watatimizo yale yote aliyoyashauri Mkuu wa mkoa,watayafanyia kazi ili halmshauri iweze kusonga mbele kuwaletea Wananchi wa Siha maendeleao

Mwisho