Site icon A24TV News

Siha awaondolea hofu Wananchi wa Kijiji cha Namwai kuhusu upatikanaji maji ya kilimo cha umwagiliaji

Na Geofrey Stephen .Arusha

Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Christopher Timbuka amesema itafikapo Agust mwaka huu wataenda kwenye vyanzo vya maji vya Somili na Urundini kuangalia upatikanaji wa maji namna gani ya ugawaji maji kati ya makundi mawili ya muekezaji pamoja na Wananchi.

Haya yamesemwa katika mkutano wa hadhara wa Wananchi Kijiji cha Namwai Wilayani humo ambapo Mkuu huyo alifika kusiliza malalamiko kwamba muekezaji wa kampuni moja ya kuku amepewa maji mengi na hofu yao kwamba maji kwenye mfereji wao wa umwagiliaji yatapungua na kusabishia mazao yao kukauka.

Mkuu huyo Akizungumza katika mkutano huo iliofanyika katika ofisi ya Kijiji hicho,amesema ifikapo Agust mwaka huu watakwenda kwenye vyanzo hivyo

“Kwa hiyo kitakachofanyika tutakwenda kwenye chanzo kuangalia kwenye vipindi vyote ,kipindi cha kiangazi na kipindi cha masika maji yanapatikana kiasi gani”amesema Timbuka.

Timbuka amesema kwa mujibu wa vibali vya watumiamaji vilivyotolewa ambavyo vinaeleza wakati wa kiangazi na wakati wa masika basi tutafuata hivyo kwamba watumia maji wanakuwa wanakaa kwa pamoja wanajadiliana kwamba kipindi hiki maji yamepungua kwa hiyo tunabana matumizi ,kwa hiyo hayo ndiyo tumekubaliana.

Kwa hiyo Wananchi waondoe wasiwasi Serikali ipo pamoja nao hasa katika kilimo hiki cha umwagiliaji cha ambacho ni cha uhakika.

Jambo jingine ambalo tumekubaliana ni kwamba wataangalia muekezaji aweze kufanya shughuli za kusaidia Jamii katika maeneo ya kijiji hicho ili kuhakikisha Wananchi wanapata maji kwa wakati wote hasa kipindi cha kiangazi wanahitaji kwa shughuli za kilimo

Afisa kilimo Wilayani humo Habibu Ally ,amesema swala la maji kupungua lengo lake moja ni kuhakikisha tunakuwa na mabwawa ya kuhifadhi maji hasa kipindi cha ukame ambacho tunazungumzia kuboresha miundombinu ya umwagiliaji ikiwamo mifereji

Hababi amesema kwa sasa katika wilaya hiyo inatekeleza Miradi ya uchimbaji visima vya kwa ajili ya umwagiliaj,kwa kuanzia imepatiwa visima 5 ,japo havitachimbwa kwenye Maeneo haya baadae watafika kwa sababu Kijiji hiki ni miongoni mwa vijiji ambavyo vipo kwenye mpango kwa sababu wakulima ni wengi na wanaari kubwa katik sekta ya kilimo.

Awali Wakazi wa Kijiji hicho Anna Laizer na Prosper Mbiga Walisema malalamiko yao kwamba mwekezaji mmoja wa kampunj ya kuku amepewa majj na kusababisha maji kwenye mfereji wao wa umwagiliaj kupungua hivyo kuhofia mazao yao kukauka

Brown Mwangoka Afisa kutoka bonde la Pangani amesema wamekubaliana na hoja ya mkuu wa wilaya kurudi kwenye vyanzo vya maji kufanya ufuatiliaji kwenye hivyo.

“Tumelichukua hilo wakati wa kiangazi tutarudi tena porini kufanya tathimini maji yanayopatikana ,hawa Wananchi wanapata maji chanzo cha Somili na muekezaji anapata maji chanzo cha Urundini “amesema Mwangoka

Mwisho