Site icon A24TV News

Siha yashika nafasi ya tatu Kitaifa ya upashaji habari

Na  bahati Hai

Halmshauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepata tuzo baada ya kumeshika nafasi ya tatu Kitaifa kwa upashaji wa habari mbali mbali za maendeleao pamoja na za kijamii katika Wilayani hiyo

Taarifa hiyo imejiri katika kikao maalumu cha Baraza la madiwani kujadili hoja za mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG), kikichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo na kuhudhuria na Viongozi mbali mbali wa serikali na Dini.

Mkurungenzi mtendaji wa halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro Haji Mnasi, katika taarifa yake kwenye kikao hicho ,amesema ushirikiano kitenge cha habari na mawasiliano ndicho kilichochngia kupata nafasi hiyo

“Ni kweli tumeoata tuzo kutokana na ushirikiano wa Afisa habari na mawasilianona wenzeke kwa namna ambavyo wanaendelea kupambana kupasha hizi habari ndiyo imetufisha kushika nafasi hiyo niwapongenze”amesema Haji

Haji amesema wilaya hii imeweza kushika nafasi hiyo tatu kitaifa katika halmshauri 184 Nchi ni jambo jema ,bahati nzuri mnakumbuka wanahabari imeweza kutolewa mbele ya Rais Samia Suluhuu Hassani

Hii ni jambo la kujivunia sana tutaendelea kushirikiana na jamii kuhakikisha wilaya yetu inaendelea kuwa imara na kuendelea katika upashaji habari mbali mbali zikiwa za Miradi,elimu,kiuchumi na kijamii

Huvyo nawaasa Watumishi kuendelea kushea habari za Siha ili mambo mazuri ya ujenzi wa Miradi ya maendeleao ikiwamo ya zahanati , shule na barabara yanayofanywa na Rais Samia Suluhuu Hassani yawe yanaonekana kwa Wananchi.

Zakayo Mosha afisa habari na mawasilianona ,amesema ushindi kwa wilaya ya siha ni ushindi kwa Wananchi wa Siha na Viongozi wake

Amesema tuzo hiyo itakuwa chachu kwa wao kuendelea kushirikiana na Wananchi kutoa taarifa mbali mbali za sio za kisherikali pekee pia za kijamii za kimaendelea.

Diwani wa kata ya Sanya juu Juma Jani,amepongeza idara hiyo kwa kufanya vizuri katika kutoa habari na kushika nafasi hiyo ambapo ameshauri waendelee na jitihada hizo
Mwisho