Site icon A24TV News

SUN KING YAZINDUA OFISI MPYA ZA KISASA ARUSHA MEYA AWAPONGEZA ,AKARIBISHA KUFUNGA MTAMBO SHULENI KWAKWE

Kampuni bora ya Nishati ya Jua ya  Sun King  ya  jijini  Arusha imezindua ofisi kubwa za kisasa ambayo ni makao makuu ya kampuni hiyo kwa Arusha huku ikiwa na mchango mkubwa kwa jamii katika Sekta ya Afya.

Akizundua ofisi hiyo Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximillian  Iranghe amepongeza uongozi wa kampuni hiyo kwa kujali na kurudisha faida wanayo pata kwa jamii kwa kuchangia mtambo mkubwa wa Sun King katika kituo cha Afya Themi  katika eneo la maabara .

Amesema kuwa , kampuni hiyo imetambua mchango mkubwa  kwa kusaidia  katika sekta ya afya pamoja na kusaidia  katika maeneo mengine mengi .

Karibu kutazama picha mbali mbali za uzinduzi wa ofisi za kisasa za Sun king .

Watumishi wa Kampuni ya Sun King wakifatilia uzinduio huo wa Ofisi zao za kisasa

Mstahiki Meya Maximillan akitambulishwa mitambo ya Sun king inavyo fanya kazi na ubora wake

Mwonekano wa Maabara ya kituo cha Themi mara baada ya kufungwa mtambo mkubwa wa Sun King.

Mwisho .