Site icon A24TV News

TANFOAM KUTIKISA NA MARATHON JIJINI ARUSHA ZAWADI NZITO NONO KWA WASHINDI

Na Geofrey Stephen Arusha

ZAIDI ya washiriki 1000 kutoka mikoa mbalimbali nchini,wanatarajiwa kushiriki kukimbia kwa kushiriki katika mbio za Tanfoam zitakazofanyia jijini Arusha,kuanzia Disemba mosi mwaka huu

Wakizungumza na vyombo vya habari  jijini Arusha katika  hafla ya uzinduzi wa mbio hizo,Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Tanfoam,Gloria Temu,amesema mbio hizo zitafanyika katika kanda tatu na wataanza na ufunguzi kwenye kanda ya kaskazini.

“Makao makuu ya mbio ni Arusha,lakini zitaongezeka kwenda kwenye mikoa mingine kwa mzunguko wa mikoa mitatu iliyoko kwenye kanda tatu nchini,ambayo ni Dodoma,Mwanza na Arusha,”alisema Gloria.

Hata hivyo,alisema lengo kuu la mbio hizo,ni kuelimisha jamii kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi na kula vizuri ili kuboresha afya na utendaji kazi.

Alisema kutakuwepo na mbio za nusu marathoni(kilomita 21),mbio za kilomita 10 na mbio za kilomita tano ambazo zitakuwa zinawahusu washiriki wanaopelendea mazoezi mepesi wakiwamo watoto na wazee.

Aidha alisema kwa washindi 10 wa mbio za kilomita 21 na 10 kwa wanawake na wanaume wote watapatiwa zawadi za fedha taslimu, huku kwa wale wa kilomita tano kwa mshindi wa kwanza mpaka watatu bila kujali jinsia nao watajipatia zawadi za pesa taslimu.

Alisema wanaotamani kushiriki mashandano hayo,zoezi la kuuza tiketi litaanza Agosti mwaka huu na utaratibu wote utapatikana kwenye tovuti ya kampuni yao.

Akizungumza wakati akizindua mbio hizo,Mbunge wa Arusha Mjini,Mrisho Gambo,amesema kwa washindi wa kwanza mbio za kilomita 21 kwa wanawake na wanaume watajishindia zawadi ya Shilingi milioni tano,medali,fulana(tisheti) na zawadi nyingine

Pia alisema kwa washindi wa pili wa kilomita 21 kwa jinsia zote, watajishindia Shilingi milioni mbili,medali,fulana na zawadi nyingine, huku washindi wa tatu wa mbio hizo watajinyakulia Shilingi milioni moja,metali na fulana.

Licha ya kuzungumza hayo,Gambo,alisema mashindano hayo yatakuwa ni fursa kwa wananchi wa Arusha,kwa kuwa kusanyiko la washiriki hao,litasaidia kuchochea uchumi kwa wakazi wa eneo hilo,kwa kuwa watanunua bidhaa mbalimbali pamoja na kufikia katika nyumba za kulala wageni.

“Linishauriana na waandaaji wa mashindano kwa kuwa yanaanzia katika uwanja wa Shekh Amri Abeid,lazima kuwepo na mabanda kwa ajili ya kutoa fursa kwa kinamama,vijana na wajisiriamali wafanye biashara ili washiriki waweze kupata huduma mbalimbali wakati mashindano yakiendelea hadi yatakapofikia tamati.

Mwisho